Pata taarifa kuu
CAR- USALAMA

UN: Juhudi zaidi zinahitajika nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati (CAR)

Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia operesheni za kulinda amani, Jean-Pierre Lacroix, amesema kuwa juhudi zaidi zinahitajika katika kuimarisha hali ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia operesheni za kulinda amani- Jean-Pierre Lacroix
Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia operesheni za kulinda amani- Jean-Pierre Lacroix © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Lacroix ameyasema haya wakati wa ziara yake jijini Bangui hapo jana ambapo pia alisisitiza umuhimu wa juhudi zaidi kufanyika ili kuhakikisha utulivu katika taifa hilo la Afrika ya kati.

“Jamuhuri ya Afrika ya Kati haitaji tena ghasia, vitendo hivi vyote vya ghasia vinakwenda kinyume na juhudi tunazofanya kuimarisha usalama na hali.” amesema Jean-Pierre Lacroix.

Nchi ya jamhuri ya Afrika ya Kati, imekuwa ikipambana na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka wa 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.