Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Vilipuzi vyaendelea kusababisha vifo, Boali yaomboleza

Mabomu ya ardhini yanaendelea kusababisha vifo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Watoto wawili wenye umri wa miaka saba waliuawa Jumapili Januari 21 katika mlipuko wa kilipuzi huko Boali, mji ulioko kilomita 95 kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Bangui. Wakiwa wameshtushwa, wananchi wengi wa Afrika ya Kati wanatoa wito wa kuanzishwa tena kwa shughuli za kutegua mabomu, ambayo zilisitishwa miaka miwili iliyopita.

Wanajeshi kutoka Kikosi cha 6 cha Territorial Intervention Brigade 6 (BIT6) cha jshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) wanashauriana kilomita 1 kutoka uwaja wa vita, huko Boali, Januari 10, 2021.
Wanajeshi kutoka Kikosi cha 6 cha Territorial Intervention Brigade 6 (BIT6) cha jshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) wanashauriana kilomita 1 kutoka uwaja wa vita, huko Boali, Januari 10, 2021. AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu huko Bangui, Rolf-Steve Domia-Leu

Kulingana na vyanzo vya ndani, mkasa huo ulitokea karibu na hoteli, hatua chache kutoka katikati mwa jiji.

"Walikuwa watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja. Wote wawili walikufa kufuatia mlipuko huo," anabainisha Pierre, meya wa Boali.

Baadhi ya wakaazi waliohojiwa na RFI wanaamini kwamba mabomi haya yaardhini yalitegwa mnamo mwaka 2020 na wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na washirika wao wa Urusi ili kuzuia kusonga mbele kwa waasi, lakini mamlaka inawanyooshea kidole wapiganaji wote.

"Wakati wa machafuko yaliyotokea hapa Boali, kulikuwa na mapigano na vilipuzi ambavyo viliwekwa na wapiganaji kutoka makundi mbalimbali. Mapigano yalikuwa mabaya sana! Kwa hivyo vilipuzi hivyo pia vilikuwa vingi katika eneo hilo," anasema Ruffin Wilibiro, kamishna wa Boali.

Sehemu ya mabomu katika eneo hilo yaliondolewa mwaka wa 2020 na kikosi cha wanajeshi wa MINUSCA, lakini mabomu hayo yanaendelea kusababisha vifo. Mkasa huu unawatia hofu baadhi ya wakazi.

“Natoa wito kwa watu kuwa watulivu. Kwa kesi kama hii, watu wako na hofu. Nina imani kwamba serikali itatuma ujumbe wa kutathmini eneo hilo ili kuona kama bado kuna mabomu yaliyotegwa au kuwekwa mahali fulani,” ameongeza Ruffin Wilibiro.

Kati ya mwaka 2021 na mwaka 2024, karibu raia thelathini walipoteza maisha kwa sababu ya vilipuzi hivi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.