Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Wakaazi wa Bangui wanakabiliwa na tatizo kubwa la mafuta

Wakazi wa Bangui wamekuwa wakiishi na shida ya mafuta kwa wiki mbili sasa. Jumla ya vituo karibu vyote vya mafuta havina bidhaa hiyo kwa kushindwa kulipa ada ya forodha na hii inasababisha uhaba wa wazalishaji wa mafuta katika mji mkuu. Gharama ya usafiri wa umma imeongezeka na hata shughuli za kijamii na kiuchumi zinaathiriwa.

Kituo cha mafuta cha TotalEnergies mjini Bangui tarehe 7 Aprili 2023.
Kituo cha mafuta cha TotalEnergies mjini Bangui tarehe 7 Aprili 2023. AFP - BARBARA DEBOUT
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Bangui, Rolf-Steve Domia-Leu

Foleni na kero sasa ni maisha ya kila siku ya watumiaji katika vituo vyote vya mafuta katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Akiwa kwenye foleni kwa siku nne, Gomez hajapata lita hata moja ya petroli. "Ili kupata mafuta, lazima ufike kwenye kituo cha mafuta karibu saa tisa usiku, usiku wa manane ... Na ili kupata bidhaa hiyo, lazima uzungumze na mhudumu kwa kumpa fedha hata kidogo," anaelezea.

Mgogoro huu unachosha, anasema Médard, mfanyabiashara ambaye anafanya kazi na kiwanda cha kusaga muhogo. "Nilinunua lita moja kwa  faranga za CFA 1,500 kutoka kwa wauzaji reja reja lakini kwa sasa inagharimu faranga za CFA 1,600 (karibu euro 2.44). Licha ya kila kitu, ubora si mzuri kwa mashine zetu na shughuli zetu zinakwenda polepole,” anasikitika.

Francis analazimika kufanya shughuli zake kwa kutembea kwa miguu kwa sababu bei ya usafiri wa umma imeongezeka kidogo. "Hali hii inaathiri raia. Teksi zimeongeza bei, pikipiki pia… Kwa hiyo, tunatembea kwa miguu,” anaeleza.

Kwa wiki mbili, vituo vya mafuta kama vile TOTAL vimefungwa na idara ya forodha kwa sababu ya kutolipa ada ya ushuru wa mafuta, gharama ambayo ni zaidi ya faranga za CFA bilioni 2 (takriban euro milioni 3). Vituo vya Tradex na Green Oil hufanya kazi mara kwa mara lakini havikidhi mahitaji ya jumla ya bidhaa za petroli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.