Pata taarifa kuu

Rekodi za joto katikati ya msimu wa baridi Morocco

Morocco inarekodi rekodi za joto msimu huu wa baridi, na mwezi wa joto zaidi wa Januari kurekodiwa katika nchi hiyo ya kifalme tangu mwaka 1940, Kurugenzi Kuu ya Hali ya Hewa (DGM) imeliambiashirika la habari la AFP siku ya Jumatano, ikihusisha hali hiyo na ongezeko la joto duniani.

Mnamo Januari, halijoto ya wastani nchini Morocco ilivunja rekodi, ikizidi viwango vya kawaida vya kipindi cha mwaka 1991-2020 kwa +3.8°C.
Mnamo Januari, halijoto ya wastani nchini Morocco ilivunja rekodi, ikizidi viwango vya kawaida vya kipindi cha mwaka 1991-2020 kwa +3.8°C. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi, ambapo joto lilikaribia 37°C hivi majuzi katika maeneo mengine, inakabiliwa na mwaka wake wa sita mfululizo wa ukame ambao unahatarisha kuwa na athari kubwa kwa kilimo, sekta muhimu ya uchumi inayowakilisha karibu 14% ya mauzo ya nje.

Mnamo mwezi wa Januari, wastani wa halijoto ulivunja rekodi, "ikizidi viwango vya kawaida vya kipindi cha mwaka wa 1991-2020 kwa +3.8°C," ametangaza Houcine Youaabed, mkuu wa mawasiliano katika DGM. Ni "mwezi wa joto zaidi wa Januari tangu vipimo vya kwanza mnamo mwaka 1940", ameliambia shirka la habari la AFP.

Rekodi za awali za kitaifa zilikuwa +2.9°C mwezi Januari 2016, ikilinganishwa na kanuni za msimu, na +1.5°C Januari mwaka 2010. Mnamo mwezi wa Februari, mikoa kadhaa iliona ongezeko la zaidi ya 10°C. C ikilinganishwa na wastani wa kawaida wa kila mwezi, kulingana na DGM.

Rekodi za kila mwezi zilivunjwa, kama vile katika mji wa pwani wa Safi (magharibi), ambao ulirekodi 35.6°C mnamo Februari 14 (ikilinganishwa na 34.7°C Februari mwaka 1960). "Matukio haya ya hivi majuzi nchini Morocco ni sehemu ya mwelekeo wa kimataifa" na "yanaonyesha matokeo ya ongezeko la joto duniani, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa," amebainisha Bw. Youaabed.

Kwa mujibu wa mtandao wa European Copernicus, katika kipindi cha kuanzia Februari 11 hadi 20, 21.6% Ulaya na kaskazini mwa Maghreb iko katika hali ya ukame, na 17.3% ya udongo unakabiliwa na upungufu wa unyevu (kitengo "onyo") na 2.5% ambapo mimea inakua kwa hali isiyo ya kawaida ("tahadhari", hali ya juu zaidi ya ukame), kulingana na hesabu zilizofanywa na shirika la habari la AFP.

Mvua inatarajiwa kurejea Morocco katika siku zijazo lakini ni mvua kubwa tu itaweza kukabiliana na upungufu huo na kunufaisha sekta ya kilimo, ambayo inaajiri karibu theluthi moja ya watu wenye umri wa kufanya kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.