Pata taarifa kuu

Malawi: Watu 6 waliuawa katika mafuriko ya wiki iliopita: Mamlaka

Nairobi – Mamlaka nchini Malawi imeripoti kuwa watu sita waliuawa wakati wengine wanne wakijeruhuiwa katika mafuriko yalioshuhudiwa katikati mwa taifa hilo wiki iliopita.

Mwaka jana kimbunga Freddy kiliripotiwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali nchini Malawi.
Mwaka jana kimbunga Freddy kiliripotiwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali nchini Malawi. AFP - AMOS GUMULIRA
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya  watu elfu kumi na nne wamepoteza makazi yao kutokana na mafuriko hayo, wengi wao wakiishi katika kambi za muda kwa mujibu wa taarifa ya idara inayoshugulika na majanga nchini Malawi.

Aidha taarifa ya idara hiyo ya majanga imeeleza kuwa sehemu kubwa ya maeneo yaliokabiliwa na mafuriko hayo bado haipitiki kutokana na uharibifu uliotokea haswa kwenye barabara na miundo mbinu nyengine.

Taarifa hiyo pia inasema kuwa kutokana na uharibifu wa miundo msingi, imekuwa ni vigumu kwa wahudumu wa mashirika ya misaada kufika katika maeneo yalioathirika.

Mafuriko hayo yamekuja ikiwa imepita mwaka moja tangu raia wa Malawi wakabiliwe na kimbuga Freddy kilichosababisha pia uharibifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.