Pata taarifa kuu

Uhalifu dhidi ya binadamu nchini Liberia: Kamanda wa zamani wa waasi ahukimiwa

Kesi katika mahakama ya Rufaa ya kamanda wa zamani wa waasi Kunti Kamara imeanza leoJumanne mjini Paris kufuatia hukumu yake ya kifungo cha maisha jela iliyotolewa mwishoni mwa mwaka 2022 kwa vitendo vya kinyama na kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia (1989 - 1997).

Aliyekuwa kamanda wa kanda wa Umoja wa Vuguvugu la Ukombozi wa Liberia kwa Demokrasia Kunti Kamara.
Aliyekuwa kamanda wa kanda wa Umoja wa Vuguvugu la Ukombozi wa Liberia kwa Demokrasia Kunti Kamara. AFP - BENOIT PEYRUCQ
Matangazo ya kibiashara

Kamanda huyu wa zamani wa kundi la Umoja wa Ukombozi kwa ajili ya Demokrasia (Ulimo) alihukumiwa kwa mara ya kwanza wakati wa kesi isiyokuwa ya kawaida nchini Ufaransa ambayo ilifanyika mwezi Oktoba na Novemba 2022.

Mahakama ya Paris ilimhukumu mwanamgambo huyo wa zamani, aliyezaliwa mwaka wa 1974, kifungo cha maisha jela kwa mfululizo wa dhuluma dhidi ya raia mwaka 1993-1994, ikiwa ni pamoja na mateso aliyofanyiwa mwalimu ambaye inadaiwa alikula nyama ya moyoni, na kwa kutokuwa na adabu katika shule, alikabiliwa na tuhuma za ubakaji wa mara kwa mara wa wasichana wawili waliobakwa na askari chini ya mamlaka yake.

Alkata rufaa, na amejikuta kwa mara nyingine tena kizimbani, akiwa amevalia koti jeusi na sura iliyodhoofika.

Alipokamatwa katika eneo la Paris mnamo Septemba 2018, Bw. Kamara alihukumiwa huko Paris chini ya "mamlaka ya ulimwengu" iliyotekelezwa, chini ya mazingira fulani, na Ufaransa kuhukumu uhalifu mbaya zaidi uliofanywa nje ya ardhi yake. Hii ni mara ya kwanza kwa utaratibu huu kutumika kwa vitendo vilivyofanywa katika nchi nyingine isipokuwa Rwanda.

Wakati wa kesi hiyo mnamo 2022, Kunti Kamara alitangaza kutokuwa na hatia na kudai kuwa mwathirika wa "njama". Wakikabiliwa na Mahakama ya Assize, walalamikaji na mashahidi kadhaa ambao walikuja hasa kutoka Liberia wamethibitisha kwamba mshtakiwa alikuwa kweli "C.O Kundi" - kwa "afisa mkuu" - ambaye alichangia kuibuka kwa utawala wa ugaidi kaskazini magharibi mwa nchi, ambayo iliangukia mikononi mwa kundila waasi la Ulimo mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Ukatili usioelezeka ulirejelewa wakati wa kesi hiyo mwanzoni: wakaazi waliouawa kwa kulazimishwa kunywa maji yanayochemka, biashara ya nyama ya binadamu, matumbo yanayotumika kama vituo vya ukaguzi, ubakaji kwa kutumia kisu cha kijeshi iliyotumbukizwa kwenye chumvi.

Kwa muda wa wiki tatu za kesi ya rufaa, mashahidi na walalamikaji watakuja tena kutoka Liberia, licha ya "mchakato wa majaribio" ambao kesi hii mpya inawakilisha, lakini kwa "matumaini kwamba itaweza kurahisisha mambo kidogojuu ya jinsi ilivyokuw ,” ameeleza mbele ya majaji mwanasheria wa pande nane za madai, Wakili Sabrina Delattre. Kesi hiyo imepangwa kuendelea hadi Machi 29.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.