Pata taarifa kuu

Liberia: Joseph Boakaï atawazwa kuwa rais wakati wa kipindi cha pili cha mpito cha amani

Rais wa Mteule wa Liberia Joseph Boakaï ameapishwa siku ya Jumatatu Januari 22 mjini Monrovia kwa muhula wa miaka sita, baada ya ushindi wake mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2023 dhidi ya nyota wa zamani wa soka na Rais anayemaliza muda wake George Weah.

Rais mteule wa Liberia Joseph Boakai wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake huko Monrovia, Liberia, Januari 22, 2024.
Rais mteule wa Liberia Joseph Boakai wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake huko Monrovia, Liberia, Januari 22, 2024. © Carielle Doe / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Maelfu ya watu walihudhuria hafla ya kuapishwa kwa raia huyo huko Capitol Building, makao makuu ya serikali, pamoja na wageni wakiwemo wakuu wa nchi jirani, hususan marais wa Sierra Leone na Ghana. Ilikuwa ni hafla muhimu kwa demokrasia changa ya Liberia.

Sherehe ya kuapishwa kwa Joseph Boakaï ilianza saa sita mchana kwa saa za huko (sawa na saa nane saa za Afrika ya Kati) katika Jengo la Capitol, makao makuu ya serikali.

Wakati wa hotuba yake, iliyochukua zaidi ya saa moja na kuzua shutuma kali kutoka kwa wachambuzi, rais huyo mpya alilazimika kutulia mara mbili kabla ya kusaidiwa kuondoka jukwaani. Mzee huyu mwenye umri wa miaka 79 alikula kiapo katika chumba cha wazi katika hali ya joto.

Baadhi ya wapinzani wa Joseph Boakai walielezea wasiwasi wao kuhusu umri na afya yake wakati wa kampeni za uchaguzi. Timu yake ilikataa ukosoaji huo na msemaji wake amesema hakuwa na maoni ya haraka kufuatia tukio hilo wakati wa sherehe.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo na ujumbe mkubwa kutoka Marekani. Pia walihudhuria marais wa Sierra Leone na Ghana, ambapo siku hii imefuatiliwa kwa umakini mkubwa, kwani Waghana watapiga kura mwishoni mwa mwaka. Pia walikuwepo mstari wa mbele: rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, pia mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mkuu wa nchi barani Afrika, ambaye alikabidhi mamlaka kwa mrithi wake George Weah mnamo 2018.

Kukabidhi mamlaka, tukio la pili katika historia ya Libeŕia kufanyika kwa amani, ni chanzo cha fahari kwa Waliberia, amesema Oscar Bloh, mwanachama wa mashiŕika ya kiŕaia.

"Hii ni siku muhimu kwa sababu, tofauti na nchi nyingine katika eneo hili, tumepitia zoezi la kukabidhiana madaraka kwa njia ya kisiasa kwa amani kutoka serikali moja iliyochaguliwa hadi serikali nyingine iliyochaguliwa kidemokrasia. Kwa hivyo Waliberia wanajivunia sana mabadiliko haya, na wana matarajio makubwa kuhusu hotuba ambayo Joseph Boakaï atatoa" , alisema hapo awali kabla ya kutawazwa kwa rais Joseph Boakaï.

Matarajio mengi katika nchi iliyodhoofishwa na ufisadi na umaskini

Kuna matarajio mengi. Kwa sababu rais mpya Joseph Boakaï anachukua mamlaka katika nchi iliyoathiriwa na umaskini na ufisadi, amesema Oscar Bloh kutoka shirika la kiraia nchini Liberia ambaye ameeleza kwa nini hii ni 'siku muhimu'.

Katika muktadha huu, mkuu mpya wa nchi Joseph Boakaï alipunguza gharama ya sherehe ya kuapishwa kwake kutoka dola 900,000 hadi dola 650,000. Kwa kupunguza matumizi, anaashiria kufutwa kwa mtindo wa mtangulizi wake George Weah, ambaye pia amehudhuria sherehe hiyo, baada ya kutetea ripoti yake siku moja kabla.

Katika siku 100, Joseph Boakaï ameahidi kutathmini mamlaka yake, pia mbele ya Waliberia.https://www.rfi.fr/sw/afrika/20240122-rais-mpya-wa-liberia-kuapishwa-mjini-monrovia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.