Pata taarifa kuu

Liberia: George Weah hatawania tena urais 2029

Nairobi – Nchini Liberia, rais George Weah ambaye alipoteza katika uchaguzi wa mwaka jana, amethibibitisha kuwa hana nia ya kugombea tena wakati wa uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka wa 2029.

Alichaguliwa katika wadhifa wa urais mwaka wa 2017 kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba dhidi ya Joseph Boakai
Alichaguliwa katika wadhifa wa urais mwaka wa 2017 kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba dhidi ya Joseph Boakai REUTERS - EDUARDO MUNOZ
Matangazo ya kibiashara

Weah, mchezaji wa zamani, alichaguliwa katika wadhifa wa urais mwaka wa 2017 kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba dhidi ya Joseph Boakai, anayetarajiwa kuapishwa Jumatatu ya wiki ijayo.

Akizungumza na waumini kanisani siku ya Jumapili, jijini Monrovia, Weah alisema kuwa atakuwa na umri wa miaka 63 katika kipindi cha miaka sita ijayo na kwamba hana nia ya kusalia katika ulingo wa kisiasa baada ya kufikisha miaka 65.

Aidha alieleza kuwa anahitaji muda wa kuwa na familia yake na wa kuangazia maisha yake.

Licha ya kutoa tangazo hilo, Weah hakusema wazi mipango yake ijayo japokuwa alisema kwamba atasaidia katika kuhubiri amani na maendeleo katika taifa lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.