Pata taarifa kuu

Cape Verde: Sita wafariki na wengine kutoweka baada ya kuzama kwa mtumbwi wa wahamiaji

Mamlaka ya Cape Verde inafanya msako siku ya Jumatatu kutafuta manusura wa mtumbwi wa wahamiaji ambao ulizama siku moja kabla kwenye kisiwa kilicho kaskazini-magharibi mwa visiwa hivi katika Bahari ya Atlantiki, ambapo watu watano wamefariki kufuatia ajali hiyo, imesema mamlaka.

Cape Verde wakati mwingine iko kwenye njia ya boti zinazobeba watu wanaohatarisha maisha yao kwenye bahari kuu ili kufika Ulaya na kuepuka umaskini.
Cape Verde wakati mwingine iko kwenye njia ya boti zinazobeba watu wanaohatarisha maisha yao kwenye bahari kuu ili kufika Ulaya na kuepuka umaskini. © Seyllou / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu watano walionusurika walikuwa kwenye mtumbwi huo wakati mtmbi huo ulipopatikana; mmoja wao alifariki hospitalini siku ya Jumatatu, na kufanya idadi ya wahzngz kufikia sita, ametangaza mjumbe wa Afya wa kisiwa cha São Vicente, Elisio Silva, kwenye televisheni ya Cape Verde.

Kulingana na maelezo ya watu wanne walionusurika, mtumbwi ambao uliondoka katika kijiji cha Mauritania ulikuwa na watu wapatao 65. "Katika siku zijazo, miili mingine inaweza kupatkana katka pwani," ameonya Bw. Silva. "Walionusurika walikabiliwa na upungufu mkubwa wa maji mwilini, lakini sasa hali zao zinaendelea vizuri na wataruhusiwa kutoka hospitali kufikia kesho," ameongeza.

Mkuu wa kikosi jamii wa eneo la kaskazini la Cape Verde, Vitória Veríssimo, amefahamisha vyombo vya habari vya eneo hilo kwamba mamlaka inakusanya data ili kutambua watu waliokuwa kwenye mtumbwi. "Nyaraka ambazo tayari zimepatikana karibu na mtumbwi huo zinaonyesha kuwa waliokuwemo wanatoka Senegal, Mauritania na Mali," amesema.

Cape Verde wakati mwingine iko kwenye njia ya boti zinazobeba watu wanaohatarisha maisha yao kwenye bahari kuu ili kufika Ulaya na kuepuka umaskini. Wanasafiri kwa boti au mitumbwi yenye injini inayotolewa na wasafirishaji-magendo wanaolipia safari hiyo. Wengi hutua katika Canary, visiwa vya Uhispania kwa lango la kuingia Ulaya.

Shuhuda nyingi zinaripoti hatari za safari, kulingana na hatari za hali ya hewa, uharibifu wa injini, kiu na njaa. Mwezi Agosti, zaidi ya wahamiaji 60 wanakisiwa kupoteza maisha ndani ya mtumbwi ambao uliondoka katika pwani ya Senegal zaidi ya mwezi mmoja kabla. Watu 38 walionusurika walipatikana.

Takriban wahamiaji 90 kutoka Senegal, Gambia, Guinea-Bissau na Sierra Leone waliokolewa katika maji ya Cape Verde katikati ya mwezi wa Januari 2023. Senegal imekumbwa na mikasa kadhaa ya uhamiaji katika miaka ya hivi karibuni, mkasa wa hivi punde zaidi ulitokea katika eneo la St. Louis siku ya Alhamisi. Takriban maiti 26 zilipatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.