Pata taarifa kuu

DRC: Familia ya Chérubin Okende, inasubiri majibu kutoka kwa mahakama ya Ubelgiji

Nchini DRC, familia ya mwaasiasa wa upinzani Chérubin Okende, aliyepatikana amefariki Julai 13, 2023 huko Kinshasa, sasa inasubiri majibu kutoka kwa yombo vya sheria nchini Ubelgiji wakati uchunguzi wa Kongo ulihitimisha mnamo Februari 29, 2024 kwamba waziri huyo wa zamani  alijiua. 

Mbunge na waziri wa zamani Chérubin Okende, Februari 25, 2023, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa.
Mbunge na waziri wa zamani Chérubin Okende, Februari 25, 2023, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa. © Pascal Mulegwa / RFI
Matangazo ya kibiashara

"Inashangaza: siku moja ya uchunguzi ili kuhitimisha kwamba mauaji yake yaliyoongozwa na mlinzi wake mwenyewe, ikifuatiwa na uchunguzi wa miezi 7 ili kuhitimisha kuwa ni aijiua? ", amesema wakili kutoka Ubelgiji wa familia ya Okende. Wakili huyo aliwasilisha malalamiko ya jinai mwezi Novemba dhidi ya mkuu wa ujasusi wa kijeshi wa DRC, Meja Jenerali Christian Ndaywel, ambaye ana uraia wa Ubelgiji.

Februari 29, 2024, mwendesha mashtaka katika Mahakama ya Juu nchini DRC alitoa hitimisho la uchunguzi wa kifo cha mpinzani Chérubin Okende. Kulingana na vyombo vya sheria vya Kongo, Chérubin Okende alijiua.

Mwili wake uligunduliwa mnamo Julai 13, 2023, kwenye gari lake lililoegeshwa kwenye barabara yenye shughuli nyingi katika mji mkuu. Jamaa ambao, leo, wanapinga hitimisho hili na sasa wanasubiri majibu kutoka kwa vyombo vya sheria vya Ubelgiji.

Ilikuwa Novemba iliyopita ambapo sehemu hii ya Ubelgiji ilianza rasmi. Wakati Maître Alexis Deswaef, wakili wa Ubelgiji wa familia ya mpinzani, alipowasilisha malalamiko ya jinai kwa jaji anayechunguza kesi dhidi ya mkuu wa upelelezi wa kijeshi wa DRC, Meja Jenerali Christian Ndaywel ambaye ana uraia wa Ubelgiji.

Kufuatia tangazo la mwendesha mashtaka mjini Kinshasa siku ya Alhamisi, Wakili Deswaef anahoji mahitimisho ya vyomo vya sheria vya Kongo. "Ni ajabu. Siku moja ya uchunguzi ili kuhitimisha kuwa ilikuwa ni mauaji ya mlinzi wake mwenyewe, ikifuatiwa na uchunguzi wa miezi 7 ili kuhitimisha kuwa alijiua? », ameongeza wakili. Nani sasa anataka kupata ripoti kutoka kwa wataalamu wa Ubelgiji waliokuja kusaidia uchunguzi huu wa Kongo. Kwa kweli, mtaalam alikuja Kinshasa kutoa msaada wa kiufundi juu ya mbinu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.