Pata taarifa kuu

Kinshasa: 'Chérubin Okende alijiua,' atangaza Mwanasheria Mkuu Mvonde

Mwendesha Mashtaka Mkuu katika Mahakama ya Juu nchini DRC, Firmin Mvonde, ametangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa siku ya Alhamisi hii, Februari 29 kwamba Chérubin Okende alijiua.

Mpinzani wa kisiasa wa Kongo Chérubin Okende, hapa ilikuwa mwezi Machi 2023, alipatikana amfariki mnamo Julai 13, 2013, mwili wake ukiwa umejaa risasi.
Mpinzani wa kisiasa wa Kongo Chérubin Okende, hapa ilikuwa mwezi Machi 2023, alipatikana amfariki mnamo Julai 13, 2013, mwili wake ukiwa umejaa risasi. AP - Samy Ntumba Shambuyi
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja ikiwa ni sehemu ya kesi inayohusu kifo cha aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, aliyepatikana amefariki kwenye gari lake Julai 13, 2023 huko Kinshasa.

Kulingana na hitimisho la uchunguzi, alijiua mwenyewe, kwa kujipiga risasi kwenye kichwa chake.

Ripoti ya uchunguzi imefuta nadharia kadhaa juu ya tukio hili. Kwanza ripoti ya uchunguzi inaeleza kuwa hayati Okende hakuwepo siku moja kabla ya kifo chake saa 10 alaasiri katika Mahakama ya Katiba (Gombe). Simu yake wakati huo ilionekana katika mtaa wa Sendwe (Kalamu).

Zaidi ya hayo, mwili wake haukuwa umejaa risasi, kama wanavyodai baadhi ya watu. "Kulikuwa na risasi moja tu," lililopigwa kutoka ndani ya gari la Cherubin Okende, ambapo hayati alipatikana akiwa amefariki akiwa peke yake kwenye kiti cha dereva, kulingana na Mwanasheria Mkuu.

Ni mwisho wa miezi mingi ya kusubiri, hasa kwa familia ya hayati Okende, ambayo ilitaka kujua ukweli wa kifo hiki cha kusikitisha.

Familia yake ikiwa imekatishwa tamaa na ucheleweshaji wa vymbo vya sheria vya DRC, ilitangaza Februari 1 uamuzi wake wa kumzika ili kufunga maombolezo, bila kungoja hitimisho la ripoti ya uchunguzi wa maiti kutoka kwa mwendesha mashtaka katika Mahakama Kuu ya Kinshasa/Gombe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.