Pata taarifa kuu

Watu 31 wafariki katika ajali ya basi iliyodondoka kutoka kwenye daraja nchini Mali

Watu 31 walifariki na kumi kujeruhiwa, baadhi yao vibaya, wakati basi lililokuwa limebeba wasafiri kuelekea Burkina Faso lilipoanguka kutoka kwenye daraja siku ya Jumanne kusini mashariki mwa Mali, Wizara ya Uchukuzi imesema.

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa 11 jioni kwenye daraja linalovuka Mto Bagoé kwenye barabara ya kitaifa nambari 7, haswa kwenye sehemu ya Niéna-Koumantou, inabainisha wizara.
Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa 11 jioni kwenye daraja linalovuka Mto Bagoé kwenye barabara ya kitaifa nambari 7, haswa kwenye sehemu ya Niéna-Koumantou, inabainisha wizara. REUTERS/Joe Penny
Matangazo ya kibiashara

"Basi (...) lililokuwa limebeba raia wa Mali na raia kutoka nchi za ukanda huo, (ambalo) lilikuwa likitoka Kéniéba kuelekea Burkina Faso, lilipinduka kutoka kwenye daraja. Sababu inayowezekana ni dereva kushindwa kulidhibiti gari", taarifa imesema.

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa 11 jioni kwenye daraja linalovuka Mto Bagoé kwenye barabara ya kitaifa nambari 7, haswa kwenye sehemu ya Niéna-Koumantou, inabainisha wizara.

Waathiriwa wanahudumiwa, ameongeza, akiwataka "madereva kuwa waangalifu na kuwa makini kwa kuwajibika kwa kazi yao".

Ajali nyingine iliua watu kumi na tano na kujeruhiwa wa kadhaa siku 46 zilizopita baada ya basi na lori kugongana katikati ya nchi. Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Mali na kwa ujumla zinatokana na ubovu wa barabara na magari, na makosa ya kibinadamu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.