Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Raia kuwachagua viongozi wapya Mei 29

Nairobi – Afrika Kusini itaandaa uchaguzi wa kitaifa na wa majimbo Mei 29, sambamba na siku ya kusherehekea miaka 30 ya uhuru na demokrasia, kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya rais ambao imesema hatua hii imeafikiwa baada ya mkuu wa nchi rais Cyril Ramaphosa kushauriana na tume ya uchaguzi kuhusu tarehe hiyo.

Rais Ramaphosa anawania kuongoza Afrika Kusini kwa muhula wa pili
Rais Ramaphosa anawania kuongoza Afrika Kusini kwa muhula wa pili AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Rais pia ameitisha kikao na wakuu wote wa mikoa na tume kujadili matayarisho ya uchaguzi huo.

Wapiga kura watakuwa wanatarajiwa kuwachagua wabunge wapya wa kitaifa pamoja na bunge la mkoa katika kila jimbo kati ya majimbo tisa nchini humo.

Rais Ramaphosa anawania kuongoza Afrika Kusini kwa muhula wa pili.

Chama chake cha African National Congress kinakabiliwa na ushindani mkali katika uchaguzi huo, huku kura za maoni zikionyesha kuwa chama hicho kinaweza kupoteza umaarufu wake kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 ya demokrasia nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1994 kufuatia kumalizika kwa mfumo dhalimu wa ubaguzi wa rangi, wakati hayati Nelson Mandela alipochaguliwa kuwa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.