Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Kinshasa na Kigali watakiwa kurejesha mazungumzo ya kujenga na ya maridhiano

Mkutano wa kilele wa usio kuwa wa kawaida kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulianza Ijumaa, Februari 16 jioni, mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia na makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU).

Mkutano huo mdogo ulitarajiwa kuwaleta pamoja viongozi wa nchi kumi na moja za Afrika, zikiwemo Afrika Kusini, Kenya, DRC, Rwanda na Tanzania pamoja na wawakilishi wa AU.
Mkutano huo mdogo ulitarajiwa kuwaleta pamoja viongozi wa nchi kumi na moja za Afrika, zikiwemo Afrika Kusini, Kenya, DRC, Rwanda na Tanzania pamoja na wawakilishi wa AU. AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

 

Mkutano huo, ulioitishwa na Mkuu wa Nchi ya Angola, João Lourenço, umejitolea kwa ajili ya kuzindua upya mchakato wa amani mashariki mwa DRC, baada ya kutumwa kwa ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ulioidhinishwa mwezi Agosti 2023, mjini Luanda.

Ilikuwa kando ya Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) unaofunguliwa siku ya Jumamosi, Februari 17 katika mji mkuu wa Ethiopia.

Mkutano huu sambamba ulifanyika mbele ya mkuu wa nchi wa DRC, Félix Tshisekedi, ambaye yuko Addis Ababa.

Kulingana na naibu mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Giscard Kusema, mkutano huu usio kuwa wa kawaida ulihusu kurejesha amani mashariki mwa DRC:

"Mkutano huu mdogo una malengo manne, ambayo ni: kurejeshwa kwa mazungumzo ya kujenga na ya maridhiano kati ya DRC na Rwanda, kusitishwa mara moja kwa uhasama, kuondolewa mara moja kwa M23 kutoka maeneo waayokalia, kuanzishwa kwa mchakato wa kuwakusanya waasi wa M23 na utekelezaji wa mpango wa kuwarejesha wawasi wa katika maisha ya kiraia na wengine kuingizwa katika vikosi vya jeshi na usalama vya taifa”.

Wakati Mkutano wa 37 wa AU ambao umefunguliwa siku ya Jumamosi mjini Addis Ababa unanuia kuiingiza DRC kwenye Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Chombo hiki cha maamuzi cha Afrika ni sawa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

DRC sasa itashiriki katika vikao vya faragha vya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, miaka 22 baada ya kutengwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.