Pata taarifa kuu

AfDB: Uchumi wa Afrika unadorora kutokana na mfumuko wa bei na kupungua kwa ukuaji mnamo 2023

Uchumi wa Afrika umedorora kutokana na mfumuko wa bei unaokadiriwa kuwa 17.8% na ukuaji uliopungua mwaka 2023, lakini bado unaendelea kustahimili, imesema Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika ripoti iliyochapishwa siku ya Ijumaa.

Jengo la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), mjini Abidjan.
Jengo la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), mjini Abidjan. RFI / Matthieu Millecamps
Matangazo ya kibiashara

 

"Wastani wa mfumuko wa bei katika bara ulikadiriwa kuwa 17.8% mwaka 2023, au asilimia 3.6 pointi zaidi kuliko mwaka 2022," inabainisha AfDB. "Mfumuko wa bei umeongezeka barani Afrika tangu kuanza kwa janga la UVIKO-19 na unaendelea kuwa juu, na kutishia utulivu wa uchumi mkuu," AfDB imeongeza.

Kulingana AfDB, "shinikizo la mfumuko wa bei limechochewa na kupanda kwa bei ya chakula na nishati duniani pamoja na mambo ya ndani kama vile ongezeko la fedha, majanga ya ugavi wa kilimo, na athari za kushuka kwa thamani ya sarafu ya taifa dhidi ya dola ya Marekani. Hata hivyo, "ukuaji barani Afrika umepungua, huku ukuaji wa pato halisi la taifa (GDP) ukikadiriwa kuwa 3.2% mwaka 2023, ikilinganishwa na 4.1% mwaka 2022," linabainisha AfDB.

Hasa, "janga la UVIKO-19", "uvamizi wa Urusi dhindi ya Ukraine" na "machafuko ya kisiasa" katika nchi kadhaa barani Afrika. Licha ya kushuka huku kwa wastani wa ukuaji wa uchumi mwaka 2023, "nchi 15 za Afrika - zikiongozwa na Ethiopia, Côte d’Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mauritius na Rwanda - zilishuhudia ongezeko la uzalishaji wa zaidi ya 5%", AfDB imeongeza.

"Tofauti kubwa kutoka nchi moja hadi nyingine"

Ukuaji mkubwa wa nchi hizi "unaonyesha athari chanya ya kuongezeka kwa matumizi ya uwekezaji, ahueni endelevu katika utalii, utendaji mzuri wa sekta ya madini na faida za mseto wa kiuchumi". Mnamo 2024, ukuaji unatarajiwa kufikia 3.8% barani Afrika, "kiwango cha jumla katika sekta zote", inasema AfDB, ambayo inakadiria kuwa "uchumi wa bara hilo unabaki kuwa thabiti".

Bara hilo pia linatarajiwa "kuwa na nchi 11 zenye uchumi mkubwa kati ya 20 unaokua kwa kasi zaidi duniani", AfDB inaongeza. Na zaidi ya hayo, "Afrika inasalia kuwa kanda ya pili inayokua kwa kasi, baada ya Asia," AfDB inabainisha.

Takwimu za 2023 na makadirio ya 2024 hazipaswi, hata hivyo, kuficha "tofauti kubwa kutoka kanda moja hadi nyingine" barani Afrika, inasema AfDB. Ili kufufua ukuaji wa Afrika, AfDB inapendekeza hatua kadhaa, ikiwa ni pamoja na "kupitishwa kwa sera za fedha" ili kupata "usawa" kati ya "kudhibiti mfumuko wa bei wa juu na kuunda motisha kwa ukuaji."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.