Pata taarifa kuu
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Benin: Gazeti la kwanza la kibinafsi lafungwa na akaunti zake kuzuiwa

Kundi la kwanza la vyombo vya habari vya kibinafsi nchini Benin, La Gazette du Golfe, lilitangaza siku ya Alhamisi kuwafuta kazi wafanyakazi wake 200 baada ya kufungiwa kwa akaunti zake za benki na mamlaka ya nchi hiyo.

Barabara yenye shughuli nyingi huko Cotonou, Septemba 2017.
Barabara yenye shughuli nyingi huko Cotonou, Septemba 2017. AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

 

"Benki zetu zimetuarifu kuwa akaunti zetu zimefungwa na taasisi za serikali (...) Hali hii inatunyima uwezo kidogo ambao tunaweza kutegemea kusaidia wafanyakazi", amesema mkuu wa La Gazette du Golfe, Ismaël Soumanou, katika barua yake ya kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi wote, ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi. "Tutatenganisha vifaa vyote vya satelaiti ikiwa ni pamoja na maji na umeme na viunganishi vya intaneti," ameongeza.

Tangu mwezi Agosti, La Gazette du Golfe, ambayo ina kituo cha televisheni, kituo cha redio na gazeti la kila wiki mbili, kilizuiwa kurusa matangazo yake kufuatia uamuzi wa Mamlaka inayosimamia na kuchunguza vyombo vya habari na mawasiliano (HAAC) iliimshutumu kwa "kukashifu mapinduzi ya serikali baada ya maoni kuhusu hali katika nchi jirani ya Niger ambapo utawala wa kijeshi ulimwondoa rais Mohamed Bazoum madarakani mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Tangu kusimamishwa huku, wafanyakazi wamepokea tu sehemu ya mishahara yao. Lakini kufungiwa kwa akaunti za benki za kundi hilo kulileta pigo kwa vyombo hivyo vitatu vya habari.

Sijui tulichosema vibaya kwenye matangazo yetu. Tuliongea kwamba kuwe na mazungumzo na sio kuingilia kijeshi nchini Niger," Valentin Adjibotcha, naibu mhariri mkuu wa zamani wa Golfe TV, ameelezea AFP. "Habari za kufukuzwa wafanyakazi kwa pamoja ni pigo", ameongeza. La Gazette du Golfe lilikuwa gazeti pekee la upinzani nchini hadi mwaka 1990.

Alipoulizwa kuhusu kufungwa kwa vyombo vya habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Rais wa Benin Patrice Talon alijibu kwamba hana uwezo wa kuchukua hatua. "Ninahisi maumivu fulani (...) Inasikitisha kwamba vyombo vya habari hivi havisikiki tena," alisema. "Mimi sio mkuu wa HAAC," mkuu wa nchi lisema, akiongeza kwamba hawezi kuingilia kazi ya HAAC.

Rais Talon, aliyechaguliwa mwaka wa 2016, kisha kuchaguliwa tena mwaka wa 2021, anashutumiwa mara kwa mara kwa kuitawala nchi hiyo kimabavu kwa niaba ya maendeleo katika nchi hii ambayo mara moja alisifiwa kwa mabadiliko ya demokrasia yake. Wanahabari kadhaa wamekamatwa nchini Benin, na mwandishi wa habari wa kigeni alifukuzwa katika miaka ya hivi karibuni kutoka nchini humo, ambapo uhuru wa vyombo vya habari "umepungua sana", kulingana na shirika la Reporters Without Borders (RSF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.