Pata taarifa kuu
UHURU-KISIASA

Mwandishi wa habari wa Benin ahukumiwa kifungo cha miezi 12 jela

Mwandishi wa habari wa Benin Virgile Ahouansè amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela siku ya Alhamisi kwa "kusambaza" habari za uwongo, baada ya kuchapishwa kwa uchunguzi kuhusu madai ya watu kuuawa wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola, kulingana na shirika la habari la AFP.

Rais Patrice Talon, aliyechaguliwa tena mnamo 2021, anashutumiwa mara kwa mara kwa kufanya mabadiliko ya kimabavu kwa niaba ya maendeleo.
Rais Patrice Talon, aliyechaguliwa tena mnamo 2021, anashutumiwa mara kwa mara kwa kufanya mabadiliko ya kimabavu kwa niaba ya maendeleo. AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

Virgile Ahouansè alikamatwa mwishoni mwa mwezi Desemba, kabla ya kuachiliwa kwa dhamana akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake mbele ya Mahakama ya Makosa ya Kiuchumi na Ugaidi (Criet), ambayo imemhukumu siku ya Alhamisi kifungo hiki na faini ya faranga za CFA 200,000 (sawa na euro 305).

"Ninaendelea kuonja uchungu wa kesi hii (...) mjadala kuhusu uhalali haujawahi kufanyika," ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu baada ya kukutwa na hatia. "Katika vikao vyote sikuwaona polisi," ameongeza.

Uchunguzi wake, uliotangazwa kwenye kituo cha redio cha Chrystal News, ambacho yeye ndiye mkurugenzi wa habari, ulidai kuwa polisi wa Benin walitekeleza mauaji katika shule ya umma katika mji mkuu Porto-Novo usiku wa Novemba 17, 2022. Wawili kati ya watu watatu waliohojiwa katika uchunguzi huu wa redio, walishuhudia mauaji haya, pia walihukumiwa siku ya Alhamisi na mahakama ya Benin kwa sababu hiyo hiyo.

Mkuu wa eneo ambako shule hii inapatikana alihukumiwa kifungo cha miezi 12 jela na faini ya faranga za CFA 200,000. Mlinzi wa shule alihukumiwa kifungo cha miezi 6 jela na faini ya faranga za CFA 100,000. Alipata uhuru wake baada ya zaidi ya miezi sita ya akizuiliwa jela.

Hukumu hizo tatu zimethibitishwa kwa shirika la habari la AFP na chanzo cha mahakama ambacho hakikutaka kutajwa jina.

Virgile Ahouansè ni mwandishi wa habari maarufu nchini Benin, ambapo alikuwa mhariri mkuu wa kituo cha redio cha Soleil Fm kinachomilikiwa na mpinzani aliye uhamishoni Sébastien Ajavon, kabla ya kufungwa na mamlaka ya Benin mwaka wa 2019. Anajulikana kwa msimamo wake dhidi ya serikali, wakati ambapo vyombo vya habari vya upinzani vimepungua katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Rais Patrice Talon, aliyechaguliwa mwaka wa 2016, kisha kuchaguliwa tena mwaka wa 2021, anashutumiwa mara kwa mara kwa kufanya mabadiliko ya kimabavu kwa niaba ya maendeleo katika nchi hii ambayo mara moja iliposifiwa kwa mabadiliko ya demokrasia yake. Wapinzani wake wakuu kwa sasa wanaishi nje ya nchi, wakilengwa na kesi mahakamani nchini Benin.

Waandishi kadhaa wa habari wamekamatwa na mwandishi wa habari wa kigeni kufukuzwa katika miaka ya hivi karibuni nchini Benin, ambapo uhuru wa vyombo vya habari "umepungua sana", kulingana na shirika la Reporters Without Borders (RSF).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.