Pata taarifa kuu

Benin yaagiza uchunguzi baada ya ghasia kuua watu 15 kaskazini mwa nchi

NAIROBI – Rais wa Benin Patrice Talon, ameagiza uchunguzi kuhusu operesheni za kijeshi zilizotekelezwa dhidi ya makundi yanayohusika na uhalifu, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Patrice Talon Rais wa Jamhuri ya Benin
Patrice Talon Rais wa Jamhuri ya Benin Sia KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Haya ni baada ya watu 15 kupoteza maisha, wengine kwa kukatwa vichwa, na sio kawaida kwa serikali kutoa taarifa kuhusu operesheni zake Kaskazini mwa Benin, lakini hii imekuwa tofauti.

Eneo la Kaskazini kama ilivyo katika mataifa ya nchi jirani, limeendelea kudhibitiwa na makundi ya kijihadi ambayo yamesambaa hadi katika nchi jirani ya Burkina Faso. 

Wahalifu wanaojihusisha na biashara haramu ya binadamu pia wamekuwa wakilengwa kwenye operesheni hiyo ya mpakani. 

Msemaji wa serikali Wilfred Houngbedji, hajaeleza kwa kina kuhusu mauaji hayo yaliyotokea, na haijafahamika iwapo makundi yenye silaha yalihusika na mauaji hayo. 

Hata hivyo, amekiri kuwa kulikuwa na changamoto ya mawasiliano kati ya maafisa wa juu wa jeshi kuhusu operesheni hiyo iliyosababisha maafa, kubaini ukweli wa tukio hilo. 

Benin inasema tangu mwaka 2021, imeshuhudia mashambulio 20 yanayotokea katika nchi jirani. 

Mwezi uliopita, rais wa Togo Faure Gnassingbe alisema kuwa wanajeshi 40 na raia 100 wameuawa katika vita alivyoviita vya kijihadi Kaskazini mwa Togo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.