Pata taarifa kuu

Mashariki mwa Sudan kutumbukia katika vita

Mashariki mwa Sudan, ambako kuna bandari na uwanja wa ndege pekee wa nchi hiyo, ambayo hadi sasa imeepushwa na vita vilivyolikumba taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika kwa zaidi ya miezi tisa, linatishia kutumbukia katika mzozo huo, kwa mujibu wa wataalamu, nchi jirani ya Eritrea inanyooshewa kidole kuchochea hali hiyo.

Vita nchini Sudan vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, wakiwemo kati ya 10,000 na 15,000 katika mji mmoja wa Darfur kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.
Vita nchini Sudan vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, wakiwemo kati ya 10,000 na 15,000 katika mji mmoja wa Darfur kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Malik Agar, nambari mbili wa utawala wa rais anayeungwa mkono na jeshi, amesema kwenye ukurasa wake wa X kwamba alizungumza na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki katikati ya mwez wa Januari kuhusu uwezo wa kuzuia vita kulikumba eneo la mashariki mwa Sudan. Tangu Aprili 15, 2023, vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohammed Hamdane Daglo na jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane wanapigana huko Khartoum, Magharibi na Kusini.

Vita hivi vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, wakiwemo kati ya 10,000 na 15,000 katika mji mmoja wa Darfur (magharibi), kulingana na wataalam wa Umoja wa Mataifa. Takriban watu milioni nane wameyakimbia makazi yao, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), wengi wakielekea katika jimbo la al-Jazeera, lango la kusini mwa Khartoum lakini pia njia ya RSF kuelekea Mashariki, ambayo ngome yake ya kihistoria ni Darfur.

Katika jimbo la al-Jazeera, RSF sasa wanapata barabara zinazoelekea katika majimbo ya Gedaref, inayopakana na Ethiopia, na Kassala, inayopakana na jimbo la Bahari Nyekundu ambako bandari ya Sudan (Port Sudan) iko, na Eritrea. Tayari katika miaka ya 1990, Khartoum ilishutumu Asmara kwa kuwafunza waasi katika ardhi yake. Lakini baadaye nchi hizi mbili ziliafikiana kuboresha maridhiano.

Lakini leo, mashahidi kadhaa waliohojiwa na shirika la habari la AFP wanadai kwamba Eritrea ina angalau kambi tano za mafunzo kwa wapiganaji wa Sudan, ikiwa ni pamoja na tatu katika eneo la Mouhib, katika eneo la Gash-Barka. Eritrea - mojawapo ya nchi zilizojitenga zaidi duniani, inayoitwa "Korea Kaskazini" ya Afrika - haijatoa maoni yoyote na imekuwa ikiomba mazungumzo ya amani tangu kuanza kwa vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.