Pata taarifa kuu

Sudan: Raia kumi wauawa katika mlipuko wa kwanza wa bomu la ardhini

Kaskazini mwa Sudan, raia kumi waliuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ardhini katika jimbo la Nile, amesema daktari ambaye aliomba kutotajwa jina.

Watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita nchini Sudan wanatembea kando ya barabara huku moshi ukifuka kwa mbali wakati wa mapigano huko Wad Madani, mji mkuu wa jimbo la al-Jazirah, Desemba 16, 2023.
Watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita nchini Sudan wanatembea kando ya barabara huku moshi ukifuka kwa mbali wakati wa mapigano huko Wad Madani, mji mkuu wa jimbo la al-Jazirah, Desemba 16, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Raia kumi waliuawa kufuatia mlipuko wa bomu la ardhini kwenye baada ya basi lililokuwa likiwasafirisha kutoka mkoa wa mashariki wa jimbo la Al-Jazeera hadi mji wa Shendi kulikanyaga," amesema daktari anayefanya kazi katika hospitali moja katika eneo hili lililo umbali wa kilomita 180 kutoka Khartoum.

Tangu Aprili 15, vita vya kugombea madaraka vimepamba moto nchini Sudan kati ya jeshi, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na wanamgambo wa Kikosi cha Rapid Support Forces (FSR) cha Jenerali Mohamed Hamdane Daglo.

Mlipuko wa bomu hilo ulilotokea siku ya Jumamosi, ni wa kwanza tangu kuanza kwa mzozo uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 13,000 nchini Sudan, kulingana na makadirio ya shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED) na zaidi ya milioni saba waliotoroka makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kwa siku kadhaa, watumiaji kwenye mitandao ya kijamii wamedai kuwa jeshi linaweka mabomu ya ardhini karibu na eneo la Shendi, madai ambayo shirika la habari la AFP linalo mwanahabari kwenye eneo hilo haijaweza kuthibitisha kwa uhuru.

Pande zinazopigana hazijatoa maoni rasmi kuhusu mlipuko huo, lakini zimeshutumiwa kwa kulipua maeneo ya raia, kulenga miundombinu na kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu.

Juhudi za kidiplomasia za mazungumzo ya amani, hasa na Marekani, Saudi Arabia na, hivi karibuni zaidi, kambi ya kikanda ya Afrika Mashariki IGAD, hadi sasa zimeshindwa.

Hata hivyo, kimsingi FSR inaonekana imechukuwa udhibiti wa maeneo mapya dhidi ya hasimu wake ambaye ni jeshi.

Wiki iliyopita, mamlaka ya Sudan na kundi la haki za kitamaduni iliripoti uvamizi wa kijeshi katika "Ufalme wa Kushi", eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO ulioko kilomita 50 kutoka Shendi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.