Pata taarifa kuu

Sudan: Mauaji kwa misingi ya kikabila yaongeza hofu ya kutokea hali mbaya Deleng

Vita ambavyo vimeingia mwezi wa kumi nchini Sudan, vinaiweka nchi hiyo kwenye hatari zisizoweza kuepukika, ikiwemo ile ya kusambaratika kabisa kwa ya usalama. Kuna dalili nyingi kwamba mgogoro unaweza kuchukua mkondo hatari. Tukio la hivi punde huko Deleng, Jimbo la Kordofan Kusini, ni mfano wa hili. Deleng ni mji wa pili kwa ukubwa katika jimbo hili katikati mwa Sudan. Imepitia dhuluma kwa misingi ya kikabila na ukoo, hali ambayo imeathiri jeshi la taifa.

Deleng, kama miji mingine mingi ya Kordofan Kusini, pia iliangukia chini ya udhibiti wa Vuguvugu la Ukombozi wa Watu wa Sudan-Kaskazini (SPLM-N), (picha ya kielelezo)
Deleng, kama miji mingine mingi ya Kordofan Kusini, pia iliangukia chini ya udhibiti wa Vuguvugu la Ukombozi wa Watu wa Sudan-Kaskazini (SPLM-N), (picha ya kielelezo) AFP - ADRIANE OHANESIAN
Matangazo ya kibiashara

 

Mji wa Deleng unakaliwa na makabila mengi ya Kiafrika ya Wanubi wanaoishi kando ya Baggaras, makabila ya Waarabu, ambao watoto wao walijiunga na jeshi kwa wingi kabla ya vita hivi.

Makabila ya Wanubi, wakiogopa mashambulizi kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), walijiweka pamoja na kuwa wanamgambo wa kujilinda. Haraka sana, wakifuata mantiki ya kikabila tu, waliwaua na kuwafukuza maofisa wa jeshi ambao hawakuwa wa makabila yao.

Wakati huo huo maafisa kutoka jamii ya Wanubi waliteuliwa kucukuwa nafasi zao. Mauaji mengine yalifanyika. Watu kadhaa waliteswa. Na nyumba zilichomwa moto kwa misingi ya ukabila. Wanubi wanasema hawana imani na jeshi, ambalo "huondoka mijini kila mara shambulio la Kikosi cha vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) linapotokea."

Deleng, kama miji mingine mingi ya Kordofan Kusini, pia iliangukia chini ya udhibiti wa kundi la Popular Liberation Movement of Sudan-North (SPLM-N), linaloongozwa na Abdelaziz el Helouambaye aliasi mwezii Juni mwaka uliyopita dhidi ya jeshi. Alichukua udhibiti wa kambi nyingi za kijeshi katika jimbo hili. Na hii licha ya makubaliano ya kimsingi ya amani yaliyotiwa saini mnamo 2020, na serikali. Anadai uhuru wa Kordofan Kusini na anataka kugawika kwa Sudan.

Hata hivyo, hali ya kibinadamu nchini humo ni ya kutisha ambapo zaidi ya watu milioni 7 waliokimbia makazi yao na wakimbizi, mfumo wa afya umedorora, maelfu ya vifo vimeripotiwa tangu kuanza kwa vita kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa FSR. Kazi ya mashirika ya misaada ya kibinadamu tayari imetatizwa na ukosefu wa usalama ulioenea, lakini inafanywa kuwa ngumu zaidi na vikwazo vya utawala vya serikali.

"Ni lazima tuweze kupata visa kwa wafanyakazi maalum wa kigeni tunaohitaji nchini Sudan. Kuna uhaba mkubwa. Kwa hiyo tunatoa wito kwa wataalam waliotoka nje ya nchi. Ni vizuizi kwa wafanyakazi wa matibabu, kwa hali ambayo inatuhusua. Vikwazo katika usambazaji wa dawa..., " amesema Jean Guy Vataux, mkurugenzi wa MSF nchini Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.