Pata taarifa kuu

Sudan: Mkuu wa jeshi aweka masharti kwa mazungumzo na mpinzani wake mkuu

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa jeshi la Sudan, ametoa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje masharti yake kwa ajili ya mazungumzo na Hemedti, ambaye anaongoza Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), makundi mawili ambayo yamekuwa yakikabiliana tangu Aprili 15, 2023.

Upande wa kushoto, mkuu wa vikosi vya jeshi la Sudan, Jenerali al-Burhan na kulia, yule wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Hemedti.
Upande wa kushoto, mkuu wa vikosi vya jeshi la Sudan, Jenerali al-Burhan na kulia, yule wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Hemedti. AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Vita vinaendelea nchini Sudan wakati mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye anaweka masharti yake ya mazungumzo na mpinzani wake Mohamed Hamdan Dogolo anayejulikana kama "Hemedti", kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (FSR). Masharti haya yametangazwa Januari 7, 2024 na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan. Kauli hii inakuja wakati Hemedti amemaliza ziara muhimu ya kidiplomasia.

Jenerali Al-Burhan anasema lazima turudi kwenye tamko la Jeddah lililotiwa saini Mei 11, 2023. "Wanamgambo wanatakiwa kwanza kuondoka katika nyumba za maelfu ya raia zinazotumiwa kama kambi za kijeshi, miji na vijiji, bado ni sharti la kuanza tena kwa mazungumzo," imeandikwa katika taarifakutoka Wizara ya Mambo ya Nje.

Wizara ya Mambo ya Nje inabainisha kwamba kujiondoa kwa RSF kutoka jimbo la al-Jazeera kusini mashariki mwa nchi kungeonyesha uzito wa wanamgambo hao katika nia yao ya mazungumzo.

Ama kuhusu tamko la Addis Ababa, lililotiwa saini wiki iliyopita na Hemedti na muungano wa vikosi vya kiraia vya Taqadum, Wizara ya Mambo ya Nje inalipuzilia mbali. Ni makubaliano yaliyotiwa saini na kundi la wafuasi wa kamanda wa RSF, imeandikwa, hali ambayo "itafungua njia kwa kugawanywa kwa mamlaka nchini Sudan kama ingetekelezwa".

Zaidi ya hayo, Wizara ya Mambo ya Nje imekasirishwa na heshima alizopewa Hemedti wakati wa mikutano yake na marais wa Kenya, Afrika Kusini na Rwanda wiki iliyopita. Mamlaka uliyo ukimbizini huko Port Sudan ilimwita balozi wake Nairobi siku ya Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.