Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano yafikia Wad Madani, jiji la makimbilio la maelfu ya wakimbizi wa ndani

Mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi minane sasa kati ya jeshi la Sudan la Jenerali al-Burhan na FSR ya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo yamefikia mji wa Wad Madani tangu Ijumaa. 

Polisi ikipiga doria mbele ya soko la Wad Madani, Juni 24, 2023.
Polisi ikipiga doria mbele ya soko la Wad Madani, Juni 24, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mji mkuu wa jimbo la al-Jazeera umekuwa ukipokea makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kwa miezi kadhaa. Kuna wakimbizi 270,000 wanaohitaji msaada, kulingana na Umoja wa Mataifa. Wad Madani iko kilomita 180 pekee kutoka mji mkuu wa Khartoum na ni eneo la kimkakati ambalo RSF inataka kudhibiti.

Vikosi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na Mohamad Hamdane Daglo tayari vina udhibiti wa miji minne mikuu na vijiji 25 mashariki mwa jimbo la al-Jazeera. Kutawala Wad Madani, mji ambao, pamoja na uzito wake wa kiuchumi na idadi ya watu, umepata umuhimu wa kimkakati unawaruhusu kupanua ushawishi wao wa kijeshi na kisiasa.

Wad Madani iko kati ya Khartoum, Darfur na Kordofan. Ni muhimu kwa kusambaza risasi na mafuta kwa FSR. Kuwa nayo huwaruhusu kuboresha hali zao na kuwa na ushawishi mkubwa katika mazungumzo yajayo.

Jiji hilo pia ni nyumbani kwa moja ya kambi muhimu za kijeshi nchini: makao makuu ya jeshi la nchi kavu. Siku ya Jumatatu, pande hizo mbili zinazokinzana zilidai kila upande kuwa zimechukua udhibiti wa kambi hiyo lakini habari hiyo haikuwezekana kuthibitishwa na chanzo huru. Katika taarifa kwenye mtandao wa X (zamani ikiitwa Twitter) wanamgambo wa RSF walidai kuwa wamechukua udhibiti wa "kambi ya kitengo cha kikosi cha nchi kavu huko Wad Madani". Kwa upande wake, jeshi linaloongozwa na Jenerali al-Burhan lilihakikisha kwamba "hali ya usalama katika jimbo la al-Jazeera imetulia", likitoa wito kwa wakaazi "kutoondoka makwao".

Wakazi na wakimbizi wamekumbwa na mzozo huo na hali hiyo imesababisha ugumu wa raia kutoka Wad Madani, jambo ambalo linatia wasiwasi Umoja wa Mataifa na taasisi za misaada ya kibinadamu.

Kulingana na vyanzo kadhaa, Abu Akla Kikel, afisa wa zamani wa jeshi anayeongoza vikosi vya ngao ya al-Jazeera, anaongoza operesheni hii. Hivi majuzi alijiunga na wanamgambo wa RSF. Wapiganaji wake hasa wanatoka katika jimbo la al-Jazeera.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.