Pata taarifa kuu
HAKI-USALAMA

Ripoti ya kutisha ya HRW yalishushia lawama jeshi la Burkina Faso kuhusu mashambulizi dhidi ya raia

Kulingana na waraka wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch (HRW) uliochapishwa jana, Alhamisi Januari 25, 2024, takriban raia 60 waliuawa katika mashambulizi ya kijeshi yaliyowasilishwa na serikali ya mpito kwama yaliwalenga wapiganaji wa kijihadi.

Wanajeshi nchini Burkina Faso (picha ya kielelezo).
Wanajeshi nchini Burkina Faso (picha ya kielelezo). © OLYMPIA DE MAISMONT AFP/File
Matangazo ya kibiashara

 

Kati ya mwezi wa Agosti na Novemba 2023, mashambulizi matatu ya anga dhidi ya maeneo ya Bouro, Bidi na Boulkessi, kaskazini mwa Burkina Faso, yalisababisha vifo vingi katika masoko au wakati wa hafla ya mazishi. Hata hivyo, kulingana na shuhuda zilizokusanywa na shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, waathiriwa hawakuwa magaidi kwa vyovyote vile.

Mbai na shutuma hizi, mwandishi wa ripoti hiyo, mtafiti IIaria Allegrozzi, aliyehojiwa na Frédéric Garat, anasema kusikitishwa na kutopendezwa kwa jumla kwa jumuiya ya kimataifa katika kile kinachotokea katika eneo hili la Sahel na anahakikishia kwamba nchi zinazoendelea kushirikiana na utawala ya kijeshi zinahusika katika mauaji hayo: "Burkina Faso leo ndio kitovu cha mzozo wa vurugu katika Sahel na hili halizungumzwi hata kidogo"

"Chukueni umakini"

"Ni mgogoro," amesema, "mgogoro uliopuuzwa kabisa na jumuiya ya kimataifa. Huu ni mgogoro uliosahaulika kwa kweli. Ni muhimu sana kutilia maanani migogoro hii kwa kuwaomba washirika wa kimataifa wa Burkina Faso kukemea hali kama hiyo, kukemea unyanyasaji unaofanywa na vikosi vya usalama. Ni wajibu kwa serikali ambazo zina ushirikiano wa kijeshi na Burkina Faso.

"Pia ninafikiria Marekani, pia anabainisha IIaria Allegrozzi, kwa sababu bado kuna sehemu ya misaada ya Marekani ambayo bado inakwenda Burkina Faso. Lakini chini ya sheria za Marekani, Marekani inapaswa kuamua kwa hakika kama ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na maafisa wa serikali ya Burkina Faso unafanyika na kama msaada unaotolewa unafuata sheria za Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.