Pata taarifa kuu

Burkina Faso yadadi kuwepo kwa njama ya kuiangusha serikali

Nairobi – Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso, imesema imezuia jaribio la kuhatarisha usalama wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Serikali inasema mpango huo unafadhiliwa na watu walio nje ya nchi hiyo
Serikali inasema mpango huo unafadhiliwa na watu walio nje ya nchi hiyo © RFI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyotumwa kwa vyombo vya habari, inawashtumu baadhi ya wanajeshi wakiwemo wale walioachishwa kazi na raia wa kawaida kupanga kushambulia taasisi za serikali.

Serikali inasema watu hao walikuwa wamepanga kuvamia kambi kadhaa za kijeshi nchini Burkina Faso, lakini wamekamatwa kabla kutekeleza mpango wao.

Aidha, serikali inasema mpango huo unafadhiliwa na watu walio nje ya nchi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mashirika ya kiraia, yanachukua madaraka kutoka kwa jeshi.

Jumapili iliyopita, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi na maafisa wa juu wa jeshi walikamatwa, wakihusishwa na jaribio la nne la kutaka kufanya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.