Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Burkina Faso: Jeshi lapokea vifaa vingi tena muhimu vya kijeshi

Nchini Burkina Faso, jeshi la taifa limepokea vifaa vipya kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi. Rais wa kipindi cha mpito, Kapteni Ibrahim Traoré, alikabidhi, Ijumaa Januari 12, kundi kubwa la silaha na magari ya kivita pamoja na risasi kwa Wizara ya Ulinzi huko Ouagadougou. Uwasilishaji ambao unafungua awamu mpya katika vita, kulingana na rais wa mpito.

Maafisa wa jeshi la Burkinabe wakipiga doria karibu na gari la kivita la Ufaransa lililoegeshwa Kaya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-kati wa Burkina Faso, mnamo Novemba 20, 2021. (Picha ya Kielelezo)
Maafisa wa jeshi la Burkinabe wakipiga doria karibu na gari la kivita la Ufaransa lililoegeshwa Kaya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini-kati wa Burkina Faso, mnamo Novemba 20, 2021. (Picha ya Kielelezo) AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Nchi anasema hili ni kundi la kwanza la vifaa vilivyopangwa na mpango wa vifaa vya kimkakati kwa majeshi ya Burkina Faso. Kapteni Ibrahim Traoré anahakikisha kwamba utoaji huu ulipatikana kutokana na michango mbalimbali kutoka kwa wananchi. Kwa mchango huu, vita dhidi ya ugaidi vinahamia hatua nyingine. "Anzisheni maendeleo yaliyosubiriwa kwa muda mrefu katika nyanja ya kivita," mkuu wa nchi amesema

“Mkikosa chochote rudieni kwangu nitajua jinsi ya kurudi kwa wananchi. Tunasubiri matokeo,” afisa mwandamizi ameviambia vikosi vya vya jeshi.

Kwa kushauri

Jenerali Kassoum Coulibaly, Waziri wa Ulinzi, amesema akiahidi, kwa niaba ya vikosi vinavyopigana, kutumia vifaa hivi kwa busara, huku akiwashukuru raia wa Burkina Faso kwa mchango wao katika "juhudi za kuleta amani", mesema.

Zaidi ya hayo, wizara yake ilifuta zorezi la kuajiri askari na mafundi 1,500 wa vyeo vya chini kwa niaba ya jeshi la kitaifa.

Saa 24 tu baada ya kuzinduliwa, mtihani huu ulifutwa na taarifa kutoka kwa jenerali. Sababu za uamuzi huu hazijaainishwa, hali ambayo inazua maswali miongoni mwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.