Pata taarifa kuu

Burkina Faso yapokea tani 25,000 za ngano kutoka Urusi

Burkina Faso imepokea siku ya Ijumaa tani 25,000 za ngano zilizotolewa na Urusi kama sehemu ya tani 200,000 zilizoahidiwa na Rais Vladimir Putin kwa nchi kadhaa za Afrika, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Moscow ilitangaza wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika mwaka 2023 kwamba itapeleka nafaka bila malipo kwa nchi sita za Afrika, ikiwa ni pamoja na Burkina Faso.
Moscow ilitangaza wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika mwaka 2023 kwamba itapeleka nafaka bila malipo kwa nchi sita za Afrika, ikiwa ni pamoja na Burkina Faso. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Vladimir Putin alitangaza wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika huko Saint Petersburg mwezi wa Julai 2023 kwamba atawasilisha nafaka bila malipo kwa nchi sita za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Burkina Faso, katika miezi ijayo. Nchi nyingine tano ni Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eritrea, Zimbabwe na Somalia.

Leo tumepokea msaada wa tani 25,000 za ngano kutoka Shirikisho la Urusi (...). Kupitia msaada huu" "Urusi inaonyesha nia yake ya kweli ya kuunga mkono juhudi za mamlaka" ya Burkina Faso ambayo "inapitia hali ngumu ya kibinadamu kufuatia mzozo wa usalama", amesema Waziri wa Mshikamano na Hatua za Kibinadamu Nandy Somé Diallo, wakati wa hafla huko Ouagadougou kuashiria mapokezi ya nafaka kutoka Urusi.

"Serikali ya Burkina Faso imefurahishwa" na "zawadi hii muhimu katika kuchangia kuwahudumia watu waliokimbia makazi yao (kutokana na vurugu za wanajihadi) na watu walio katika mazingira magumu," ameongeza, akihakikishia kwamba tani hizi 25,000 za ngano zitatumiwa "kwa busara".

Msaada huu "ni ishara kubwa ya nia ya" Rais wa Urusi "kutoa msukumo mkubwa kwa ushirikiano na Burkina Faso, mmoja wa washirika wetu wa kimkakati katika bara la Afrika," ametangaza Alexei Saltykov, balozi wa Urusi nchini Côte d'Ivoire mwenye makaazi yake nchini Burkina Faso.

"Msaada huu lazima usiwe sehemu ya mzunguko usio na mwisho wa michango. Ni lazima utupatie changamoto kuhusu kazi ya haraka, muhimu na ya lazima kwa ajili ya maendeleo ya uwezo wetu wa uzalishaji ili kuondokana na utegemezi wa chakula  kutoka nje", amesema Karamoko Jean Marie Traoré, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso.

Urusi ilifungua tena ubalozi wake nchini Burkina Faso mwishoni mwa mwezi wa Desemba, ambao iliufunga mwaka 1992, hivyo kuendeleza uhusiano na nchi hii ya Sahel inayoongozwa na utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi ya Septemba 2022 na ambayo inataka kubadilisha ushirikiano wake tangu ilipojitenga na Ufaransa.

Urusi pia inachukua fursa ya kujiondoa kwa Ufaransa nchini Burkina Faso, Mali na Niger, pia zikiongozwa na tawala za kijeshi, kutoa msaada wa kiulinzi kwa nchi hizi katika mapambano yao dhidi ya makundi ya kijihadi yenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.