Pata taarifa kuu

Urusi yafungua tena Ubalozi wake nchini Burkina Faso

Urusi imefungua tena ubalozi wake nchini Burkina Faso baada ya miaka 32.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alipokutana na kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traore jijini Saint Petersburg mwezi Septemba  2023
Rais wa Urusi Vladimir Putin alipokutana na kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Ibrahim Traore jijini Saint Petersburg mwezi Septemba 2023 via REUTERS - TASS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya taifa hilo la Afrika Magharibi, kuharibika kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa, iliyokuwa koloni yake.

Wizara ya Mambo ya nje ya Burkina Faso, imethibitisha kufunguliwa tena kwa Ubalozi wa Urusi  jijini Ouagadougou kuanzia siku ya Alhamisi.

Ubalozi wa Urusi nchini Cote Dvoire, Alexei Saltykov, amesema kwa sasa atakuwa Balozi wa nchi yake nchini Burkina Faso hadi pale Moscow itakapomtuma Balozi mpya jijini Ouagadougou.

Saltykov, ameelezea hatua ya kurejeshwa kwa Ubalozi huo kwa sababu ya urafiki wa siku nyingi na kuelezea Burkina Faso kama mshrika wa karibu.

Baada ya Burkina Faso kupitia mapinduzi ya kijeshi mara mbili, uongozi wa kijeshi umekuwa karibu na Urusi na kuachana na Ufaransa.

Mwezi Oktoba, nchi hizo mbili zilitiana saini mkataba wa Urusi  kujenga kiwanda cha nishati cha nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.