Pata taarifa kuu

Madagascar: Mvua kubwa husababisha uharibifu mkubwa na watu kutoroka makazi yao

Kimbunga Belal kilichopiga Reunion na Mauritius wiki hii laki hakijapiga nchini Madagascar. Lakini kwa upande wake, nchi hii imekuwa inakabiliwa na mvua kubwa hasa tangu Jumatatu. Sehemu kubwa ya kisiwa imeathiriwa - isipokuwa Kusini na Kusini-Magharibi. Mvua hizi zenye upepo mkali, zinazoambatana na mawingu makubwa, zitaendelea Jumapili hii, Januari 21.

Madagascar imenusurika na kimbunga Belal kilichopiga Reunion na Mauritius wiki hii, lakini nchi hii inakabiliwa na mvua kubwa. (picha ya kielelezo)
Madagascar imenusurika na kimbunga Belal kilichopiga Reunion na Mauritius wiki hii, lakini nchi hii inakabiliwa na mvua kubwa. (picha ya kielelezo) AFP - LAURA MOROSOLI
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwandishi wetu wa Antananarivo, Pauline Le Troquier

Katika siku nne, mvua kubwa iliyonyesha nchini Madagascar iliwafanya karibu watu 1,600 kuyahama makazi yao, wengi wao ni kutoka Kaskazini katika mikoa ya Boeny na Sofia. Tangu kuanza kwa mvua hiyo, barabara na nyumba kadhaa zimesombwa na maji. 

Ofisi ya Kitaifa ya Kukabiliana na Hatari na Majanga (BGNRC) tayari inasema watu wawili hawajulikani waliko na karibu watu 3,400 waliathiriwa na mvua za awali.

“Mvua ni nyingi hadi maji yanaingia ndani ya nyumba, hizi ni nyumba ambazo ziko kwenye makazi duni. Kuna madaraja ambayo hatuwezi kuvuka tena kwa sababu kuna maji mengi. Katika vichochoro au njia ambazo zimemezwa na matope, kuna matope mengi na hatuwezi tena kupita, " amesema Sandrine, mkazi wa kisiwa cha Nosy Be.

Hali ambayo ilizorotesha sehemu ya kisiwa hicho katika siku za hivi karibuni, na hivyo kusimamisha shughuli za shule katika maeneo mengine.

Kwa sasa, uharibifu huo unaenea hadi mikoa 9 kati ya 23 ya Madagasar. Barabara nne hazipiti kwa sasa baada ya kukatika kutokana na maji. Katika eneo la Boeny, bwawa la kilimo cha maji lilibomoka baada ya mafuriko. Huko Ambatondrazaka, ghala la mpunga la Madagascar, makumi ya heka za mashamba ya mpunga yameharibiwa.

Katika saa zijazo, raia wa Madagascar wanatakiwa kuwa macho. Kabla ya hali ya hewa kurejea kuwa sawa siku ya Jumatatu, Januari 22, "lazima tutarajie dhoruba kali karibu kila mahali nchini," anaonya Lovandrainy Ratovoarisoa, mtabiri wa hali ya hewa nchini Madagascar.

Hasa, eneo la Diana kaskazini liko kwenye tahadhari ya manjano ya "mvua kubwa". Wakaazi wake tayari wanaombwa kuhama maeneo ambayo huenda yakakumbwa na mafuriko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.