Pata taarifa kuu
DINI-MAADILI

Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Senegal wanakataa kuwabariki wapenzi wa jinsia moja

Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Senegal wameelezea kukataa kwao kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, kama Vatican ilivyoidhinisha hivi karibuni chini ya masharti.

Mabadiliko ya kimafundisho yaliyohimizwa na Papa Francis yamechochea kutokubaliwa kwa viongozi wengi wa Kanisa Katoliki barani Afrika, wakiungana na wale wa Senegal.
Mabadiliko ya kimafundisho yaliyohimizwa na Papa Francis yamechochea kutokubaliwa kwa viongozi wengi wa Kanisa Katoliki barani Afrika, wakiungana na wale wa Senegal. © YouTube / Travaux BRT Dakar
Matangazo ya kibiashara

 

Katika waraka uliochapishwa tarehe 18 Desemba na kuidhinishwa na Kiongogozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, dicastery (huduma) ya Mafundisho ya Imani iliidhinisha baraka za wanandoa "wasio wa kawaida" machoni pa Kanisa, wakiwemo waliofunga ndoa tena na wanandoa wa jinsia moja, mradi inatolewa nje ya matambiko ya kiliturujia. Kile ambacho kinaonekana kuwa mabadiliko ya kimafundisho yaliyohimizwa na Papa Francis yamechochea kutokubaliwa kwa viongozi wengi wa Kanisa Katoliki barani Afrika, wakiungana na wale wa Senegal.

Katika muktadha wa sasa wa uhalalishaji unaoendelea na wa hila au uhalalishaji wa ushoga na upotovu mwingine wa kimaadili, sisi, wachungaji wenu, maaskofu wa Senegal, tunathibitisha kwa uwazi kwamba, katika dayosisi zetu, hakuna aina ya baraka za kiliturujia au za ziada za kiliturujia haziwezi kutolewa kwa watu wawili wa jinsia moja ambao wanaomba waziwazi kama wanandoa", ameandika askofu mkuu wa Dakar na maaskofu wa Senegal katika taarifa ya Alhamisi na kutumwa kwa shirika la habari la  AFP siku ya Ijumaa.

Ushoga unaelezewa kama "mkengeuko wa maadili wa wakati wetu". “Mikengeuko ya kimaadili, kwa ujumla, na hasa ushoga katika usemi wake mbalimbali, inachukuliwa, katika Kanisa, kama chukizo dhidi ya mapenzi ya Mungu,” wasema maaskofu, huku wakisisitiza umuhimu wa “hangaiko la Kanisa kwa kila mtu. .. bila kujali chaguo lao na mwelekeo wa maisha". Kuhusu kuishi tena pamoja au waliotalikiana waliofunga ndoa tena, "fundisho la Kanisa halipaswi kubadilishwa kwa njia yoyote," wamesema.

Kongamano la Mabaraza ya Maaskofu ya Afrika na Madagascar (SEEAM), ambalo linawakilisha Maaskofu wa Kikatoliki wa bara hilo, tayari lilitangaza Januari 11 kwamba baraka ya wapenzi wa jinsia moja "haifai" katika Afrika. Baraka kama hiyo "itakuwa inakinzana moja kwa moja na maadili ya kitamaduni ya jumuiya za Kiafrika," SECAM ilisema.

Takriban mataifa thelathini ya Kiafrika, kati ya takriban hamsini kwa jumla, yanakataza ushoga, kulingana na Jumuiya ya Kimataifa ya Wasagaji, Mashoga, Wapenzi wa Jinsia Mbili, Wanaoshiriki Jinsia Moja (ILGA). 

Nchini Senegal, ushoga unachukuliwa kuwa upotovu. Sheria inaadhibu kile kinachoitwa "vitendo visivyo vya asili na mtu wa jinsia moja" kwa kifungo cha mwaka mmoja hadi mitano. Jumuiya ya Kikatoliki ya Senegal inaishi kwa maelewano makubwa na Waislamu walio wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.