Pata taarifa kuu

Mmarekani wa pili akamatwa nchini Libya kwa kuwadili watu kwa imani ya Kikristo

Mmarekani wa pili, mwalimu wa Kiingereza huko Tripoli, nchini Libya, amekamatwa kwa kuwabadili watu kwa imani ya Kikristo, idara ya usalama ya Libya imesema hivi punde, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwa Mmarekani kwa sababu hiyo.

Maafisa wa Polisi kwenye kituo cha ukaguzi huko Tripoli.
Maafisa wa Polisi kwenye kituo cha ukaguzi huko Tripoli. REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Idara ya Usalama wa Ndani (OSI) imesema katika taarifa yake kwamba imemkamata "S.B.O., wa uraia wa Marekani", naibu mkurugenzi wa kituo cha kufundisha lugha huko Tripoli, na ambaye anafanya kazi "pamoja na mke wake, kama mmishonari kwa niaba ya Kusanyiko la Assemblies of God ili kuwapotosha wana wa watu wetu wa Kiislamu." "Assemblies of God", ni shirika la wamisionari lililoanzishwa katika Jimbo la Arkansas nchini Marekani mwaka wa 1914.

Siku ya Jumatano OSI ilitangaza kukamatwa kwa Mmarekani wa kwanza wa Mkristo aliye kuwa akijaribu kuwabadili raia wa Libya kwa imani ya Ukristo, pia mwalimu katika kituo hicho cha lugha. Jina lake halikutajwa, lakini vyombo vya habari vya Libya vilimtambulisha kama Jeff Wilson, mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya huduma za ushauri ya Libya Business.

Katika taarifa ya Alhamisi kwa vyombo vya habari, OSI pia ilitangaza kukamatwa kwa Walibya wawili, ikiwa ni pamoja na "msichana mwenye umri wa miaka 22, aliyesilimu akiwa na umri wa miaka 15" na ambaye anasimulia kwenye video ambapo anaonekana na uso wake kuwa na giza jinsi yeye alivyokuwa "mmishonari" na kuwajibika kwa "kuwaajiri vijana wa Libya".

Raia kadhaa wa Libya walikamatwa hivi majuzi kwa kubadili dini, ukengeufu na kukuza imani ya kuwa hakuna Mungu na walirejelea upande wa mashtaka baada ya kukiri kurekodiwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, kufuatia machafuko ya nchi za Kiarabu, Libya imetumbukia katika machafuko na mgawanyiko. Serikali mbili zinagombania madaraka, moja ikiwa na makao yake makuu mjini Tripoli (magharibi) na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine ikiwa mashariki na kuungwa mkono na kambi ya Marshal Khalifa Haftar na Baraza la Wawakilishi.

Uislamu ndio dini rasmi nchini Libya. Wasio Waislamu nchini humo ni wageni, wengi wao wakiwa Wakristo, ambao wana uhuru wa kuabudu makanisani hasa mjini Tripoli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.