Pata taarifa kuu

UN: Balozi wa serikali ya mpito ya Niger ruksa kuiwakilisha Niamey New York

Baada ya sintofahamu kwa miezi mitatu, Tume maalumu ya Umoja wa Mataifa imechukuwa uamuzi. Balozi wa serikali ya mpito ya Niger sasa ataweza kuiwakilisha Niamey mjini New York. Mwezi wa Septemba mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulimpiga marufuku kuingia kwenye Baraza Kuu, kwa kuzingatia maagizo yaliyotolewa na Baraza la Usalama ambalo liliendelea kutambua serikali ya Mohamed Bazoum kama serikali pekee halali.

Tume ya Hati za Utambulisho, ambayo hukutana mara moja kwa mwaka mjini New York ili kutoa uamuzi kuhusu mizozo inayoweza kutokea kuhusu utambuzi wa uhalali wa mabalozi katika Umoja wa Mataifa, iliamua tarehe 6 Desemba kumtambua balozi wa Niger wa serikali ya mpito.
Tume ya Hati za Utambulisho, ambayo hukutana mara moja kwa mwaka mjini New York ili kutoa uamuzi kuhusu mizozo inayoweza kutokea kuhusu utambuzi wa uhalali wa mabalozi katika Umoja wa Mataifa, iliamua tarehe 6 Desemba kumtambua balozi wa Niger wa serikali ya mpito. © Eduardo Munoz / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Ni mazungumzo ambayo yanapata pointi kwa serikali ya Jenerali Tiani, na ambayo nyuma ya pazia yanaonyesha jinsi serikali ya mpito ya Niger inavyojiimarisha katika Afrika Magharibi.

Tume ya Hati za Utambulisho, ambayo hukutana mara moja kwa mwaka mjini New York ili kutoa uamuzi kuhusu mizozo inayoweza kutokea kuhusu utambuzi wa uhalali wa mabalozi katika Umoja wa Mataifa, iliamua tarehe 6 Desemba kumtambua balozi wa Niger wa serikali ya mpito.

Aliteuliwa na Mohamed Bazoum, kisha akakataliwa naye alipojiunga na wanajeshi waliofanya mapinduzi, na hivyo kusababisha kutokuwa na uhakika juu ya uhalali wake katika Umoja wa Mataifa. Urusi, China na Marekani, watatu kati ya wanachama tisa wa Tume hiyo, awali walidhani kutotoa uamuzi juu ya suala la Niger na kuacha kiti tupu kwa Niger katika Umoja wa Mataifa. Lakini Togo na Nigeria, wanachama wengine wawili ambao wanaonekana wamebadili msimamo wao katika wiki chache dhidi ya Jenerali Tiani. Wameshinikiza mamlaka hizo tatu kumtambua rasmi mwakilishi wake.

Maelewano ya hivi majuzi kati ya Niamey na Moscow kufuatia ziara ya Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi nchini niger mnamo Desemba 4 yanaweza kuwa yameishawishi Urusi kutoa nguvu hii kwa Umoja wa Mataifa. Maamuzi yakifanywa kwa maafikiano na Marekani ikiwa haijapokea mwongozo wowote maalum wa kupinga, uamuzi huo uliidhinishwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.