Pata taarifa kuu

Marekani yajaribu bila mafanikio kubadilisha msimamo wa nchi za ECOWAS nchini Niger

Huko New York, kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Marekani ilijaribu kuzishawishi nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kupunguza msimamo dhidi ya viongozi wa mapinduzi nchini Niger. Kauli hiyo ilitolewa siku ya Ijumaa asubuhi wakati wa mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Lakini ni wazi, hoja hiyo haikufanikiwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa jukwaani wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 24, 2019.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa jukwaani wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 24, 2019. AP - Mary Altaffer
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko New York, Christophe Boisbouvier

Kuanzia Jumatatu wiki hii, katika barabara za Umoja wa Mataifa mjini New York, wanadiplomasia wa Marekani waliwasogelea wenzao wa Afrika Magharibi nchini Niger na kujaribu kuwafanya waidhinishe mpango wa kumaliza mgogoro huo, kwa kuzingatia maelewano na viongozi wa mapinduzi wa Niamey.

Na ili kufanya hivi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitarajia kuweza kuwaleta pamoja karibu naye jana asubuhi wakuu kadhaa wa nchi za Afrika Magharibi kama vile Bola Tinubu wa Nigeria na rais wa Senegal Macky Sall. Jibu lililoratibiwa kutoka kwa viongozi wa nchi za Afrika Magharibi: "Msimamo wetu juu ya mapinduzi ya mwezi wa Julai nchini Niger uko wazi, ulifafanuliwa katika mkutano wa mwisho wa wakuu wa nchi wa ECOWAS na sio Antony Blinken ambaye ataubadilisha."

Kutokana na hali hiyo, jana asubuhi, hakuna rais wa Afrika Magharibi aliyeitikia mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani. Wakuu wa nchi za ECOWAS waliwakilishwa na mawaziri wao wa mambo ya nje. Na kutokana na msimamo wa viongozi hao wa nchi za Afrika Magharibi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani alitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo aliitaka serikali ya Niamey kumwachilia huru rais Mohamed Bazoum na kumruhusu kurejea kwenye mamlaka yake kama mkuu wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.