Pata taarifa kuu

Niamey yamtaka mratibu wa Umoja wa Mataifa kuondoka nchini Niger ndani ya saa 72

Utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi nchini Niger umeagiza mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Niger, Louise Aubin, kuondoka nchini humo ndani ya saa 72, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotangazwa Jumanne na kutumwa kwa shirikala habari la AFP siku ya Jumatano. 

Waziri Mkuu mteule wa Niger Ali Mahamane Lamine Zeine akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Niamey, Niger, Septemba 4, 2023.
Waziri Mkuu mteule wa Niger Ali Mahamane Lamine Zeine akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Niamey, Niger, Septemba 4, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa kijeshi unalaani "vizuizi" vilivyowekwa,na Umoja wa Mataifa "kuzuia ushiriki" wa Niger katika Mkutano Mkuu wa umoja huo mnamo mwezi wa Septemba.

Hivi karibuni Utawala wa kijeshi ambao ulichukua mamlaka huko Niamey mnamo Julai 26 ulimpa balozi wa Ufaransa nchini Niger masaa 48 kuondoka nchini humo licha ya kutupuliwa mbali na serikali ya Ufaransa ikidai kwamba hitambui utawala huo, kabla ya kurejelea uamuzi wake na kumuondoa balozi Bw. Sylvain Itte nchini humo na kumejesha nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.