Pata taarifa kuu

Kundi la kwanza la wanajeshi wa Ufaransa waondoka Niger

Mvutano kati ya Niger na Ufaransa umefungua ukurasa mpya baada ya kundi la kwanza la wanajeshi wa Ufaransa kuanza kuondoka nchini Niger wakisindikizwa na vikosi vya nchi hiyo, kutoka magharibi mwa nchi kuelekea mahali panapoweza kuwa Chad, kulingana na vyanzo kadhaa vya usalama.

Takriban wanajeshi 1,400 wa Ufaransa na wanajeshi wa jeshi la anga wametumwa nchini Niger kusaidia waajeshi wa Niger kupigana dhidi ya wanajihadi nchini humo.
Takriban wanajeshi 1,400 wa Ufaransa na wanajeshi wa jeshi la anga wametumwa nchini Niger kusaidia waajeshi wa Niger kupigana dhidi ya wanajihadi nchini humo. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa kijeshi nchini Niger uliitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake baada ya kuingia madarakani kwa mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai, na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza kuanza kuondoka kwa wanajeshi hao mwishoni mwa mwezi Septemba.

Takriban wanajeshi 1,400 wa Ufaransa na wanajeshi wa anga wametumwa nchini humo kusaidi jeshi la Niger kupigana dhidi ya wanajihadi. Ufaransa ina wanajeshi karibu 1,000 huko Niamey na 400 kwenye kambi mbili maarufu magharibi mwa nchi, huko Ouallam na Tabarey-Barey, katikati mwa nchi, eneo linaloitwa "mipaka mitatu" pamoja na Mali na Burkina Faso.

Msafara wa wanajeshi kutoka Tabarey-Barey uliwasili Niamey siku ya Jumanne mchana, ukiwa na magari makubwa ya mizigo yaliyobeba vifaa na magari ya kivita, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

"Kuondoka kwa kundi la kwanza la wanajeshi wa Ufaransa kunafanyika, kwa mujibu wa mipango na uratibu unaoendelea," AFP ilifahamu mapema kutoka kwa majeshi ya Ufaransa, na kuthibitisha tangazo lililotolewa siku moja kabla na utawala wa kijeshi wa Niger, ambao ulitaja misafara inayosindikizwa na jeshi lake bila kutaja wapi inaelekea.

Ndege iliyo na vifaa vya Ufaransa na kundi la kwanza la wanajeshi wanaopewa kipaumbele (kitengo kinachohusika na matibabu, hasa) pia iliondoka Niamey siku ya Jumatatu, kulingana na shirika la habarila AFP, likinukuu chanzo kingine cha kijeshi.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na suala hilo, wanajeshi hao wanakwenda Chad, wakitumia barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,600 hadi kufika N'Djamena, ambako ndiko kunakopatikana komandi ya vikosi vya Ufaransa katika ukanda wa Sahel. Siku ya Ijumaa utawala wa kijeshi ulitangaza kwamba zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa litafanyika "kwa usalama kamili".

Safari hatari

Baada ya Ufaransa kuondoka nchini Mali, kisha Burkina Faso kuanzia majira ya joto ya mwaka 2022, Niger imekuwa mshirika mkuu wa operesheni za Ufaransa za kupambana dhidi ya wanajihadi, katika eneo ambalo makundi yenye silaha yanashirikiana na Islamic State na Al-Qaeda. Kuondoka huku kunawapa wanajeshi wa Ufaransa changamoto maradufu ya vifaa na usalama.

Chaguo za usafiri ni chache, tena hatari, pamoja na hatari ya maandamano dhidi ya Ufaransa lakini pia kuwepo kwa wanajihadi wanaohusishwa na Boko Haram na ISWAP kundi lenye mafungamano na IS katika eneo la Diffa (mashariki) ya Chad).

Mipaka ya ardhi ya Niger na Benin na Nigeria pia imefungwa tangu mapinduzi ya Julai 26 yaliyomuondoa madarakani rais Mohamed Bazoum, mshirika wa Ufaransa. Na Niger imepiga marufuku ndege za kiraia na za kijeshi za Ufaransa kuruka juu ya anga ya ardhi yakei, isipokuwa kama zitaruhusiwa. Hata hivyo, mipaka imefunguliwa tena na Algeria, Libya, Burkina Faso, Mali na Chad.

Ikiwa makontena ya Ufaransa yatasafirishwa hadi Chad, safari itakuwa ndefu, ngumu na ya hatari. Kisha watalazimika kupitia bandari ya Douala, nchini Cameroon, mwishoni mwa msafara mwingine mgumu, kulingana na chanzo kilicho karibu na suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.