Pata taarifa kuu

Niger: Zoezi la kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa litafanyika ndani ya miezi mitatu

Kwa kumaliza mzozo wa miezi miwili na utawala wa kijeshi wa Niger, rais Emmanuel Macron alitangaza siku ya Jumapili kurejea nyumbani kwa balozi wa Ufaransa nchini Niger na kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger "mwishoni mwa mwaka huu". Taarifa kuhusu kurejeshwa nyumbani kwa wanajeshi 1,500 wa Ufaransa waliopo Niger.

Wanajeshi wa Ufaransa wakikagua ndege isiyo na rubani ya Reaper katika kambi ya kikosi cha wanaanga wa Ufaransa cha BAP huko Niamey mnamo Mei 14, 2023.
Wanajeshi wa Ufaransa wakikagua ndege isiyo na rubani ya Reaper katika kambi ya kikosi cha wanaanga wa Ufaransa cha BAP huko Niamey mnamo Mei 14, 2023. AFP - ALAIN JOCARD
Matangazo ya kibiashara

Mipango madhubuti itakuwa ufunguo wa kuondoka Niger ndani ya miezi mitatu pekee. Kuhusu jeshi la Ufaransa, tunakumbuka kwamba kwa wiki kadhaa tayari, mawasiliano yamefanywa na wenzao wa Niger kujiandaa kwa zoezi hili kuondoka nchini humo. Wanajeshi 200 walioko Ouallam, huko Liptako nchini Niger, watajiunga na kambi ya kikosi cha wanaanga cha Niamey, ambako kunapatikana idadi kubwa ya wanajeshi wa Ufaransa. Kufuatia safari za ndege za kila mara, basi itakuwa rahisi kurudisha wanajeshi Ufaransa.

Kwa upande mwingine, ili kuondoa vitu vizito kama vile magari ya kivita, helikopta na vitu vingie, wataalamu wa jeshi la Ufaransa watalazimika kuandaa misafara mikubwa ya ardhini kufikia bandari za Cotonou au Abidjan. Kisha wataingia nchini Ufaransa kwa boti kwa sababu hakuna mipango ya kupeleka tena vifaa kwenye kambi nyingine za kijeshi za Ufaransa barani Afrika.

Wahandisi sasa wana uzoefu katika hatua hizi kubwa. Mnamo 2022, kikosi cha Barkhane - wanajeshi 4,500 - waliweza kuondoka Mali katika kipindi cha miezi sita. Changamoto halisi ya vifaa ambayo italazimika kufanywa upya hata kama wakati huu, hali si shwari.

Chad, kituo cha mwisho cha jeshi la Ufaransa huko Sahel

Katika majira ya kiangazi ya 2022, kuondoka huku kwa kikosi cha Barkhane kutoka Mali tayari kulikuwa karibu kukomesha uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa katika eneo la Sahel kwa sababu wanajeshi 4,500 waliokuwa wakipigana huko walirudi Ufaransa. Nchini Niger, idadi ya wanajeshi wa Ufaransa haijawahi kuzidi askari 1,500, wengi wao wakiwa kwenye kambi ya 101 ya kikosi cha wanaanga huko Niamey. Kikosi kikubwa kinaundwa na ndege na mafundi wa kuhudumia ndege tatu aina ya Mirage 2000 na ndege 6 zisizo na rubani aina ya Reaperi.

Hata hivyo, Ufaransa ilibakia kuwa nchi pekee iliyoipa mamlaka ya Niger ushirikiano wa kivita: wanajeshi wa Ufaransa walikuwa katika huduma ya vikosi vya jeshi vya Niger ambavyo pekee vilipanga operesheni. Kwa hivyo, askari 200 wa Ufaransa walichukua zamu kila baada ya miezi minne huko Ouallam, na katika eneo la Liptako kulinda mpaka na Mali na vikosi vya Niger.

Tofauti na Wafaransa, wanajeshi wa Italia, Wajerumani na Wamarekani waliopo Niger kila mara wamekuwa wakifanya mafunzo tu. Jeshi la Marekani pia hurusha ndege zake zisizo na rubani kutoka kituo cha Agadez, lakini kwa mfuko wake.

Kwa kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger, Chad kwa hiyo inasalia kuwa ngome ya mwisho ya jeshi la Ufaransa katika eneo la Sahel. kikosi hiki chenye wanajeshi 1,000, kambi ya wanajeshi wa anga na makao makuu huko Ndjamena na uwanja wa uchunguzi ambao sasa unaishia kwa ukanda wa mashariki mwa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.