Pata taarifa kuu

Niger: Emmanuel Macron atangaza kurejea nchini kwa balozi wa Ufaransa 'katika saa zijazo'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Jumapili hii jioni kwenye televisheni ya TF1 na France 2 kurejea nchini "katika saa zijazo" kwa balozi wa Ufaransa huko Niamey, na kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Emmanuel Macron kwenye kwenye televiseni ya TF1 na France 2, Septemba 24, 2023.
Emmanuel Macron kwenye kwenye televiseni ya TF1 na France 2, Septemba 24, 2023. AFP - GEOFFROY VAN DER HASSELT
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa imeamua kumrejesha nyumbani balozi wake, ambaye hadi sasa Paris ilikuwa inakataa kumrejesha, na "tunasitisha ushirikiano wetu wa kijeshi na Niger", amesema Emmanuel Macron katika mahojiano ya televisheni, akibaini kwamba wanajeshi 1,500 wa Ufaransa wataondoka "katika majuma na miezi ijayo” na kwamba kuondoka kwa wanajeshi hao kutakamilika kabisa “mwishoni mwa mwaka”.

"Hakuna tena ushirikiano kati ya Ufaransa na Afrika

Uwepo wa Ufaransa nchini Niger, hata hivyo, umehalalishwa hadi sasa, kulingana na Emmanuel Macron "kwa sababu ya ombi la nchi kadhaa na kanda, tumekuwa tukipambana na ugaidi." Rais wa Jamhuri pia amekaribisha kujitolea kwa wanajeshi wa Ufaransa katika Operesheni Barkhane.

"Hakuna tena ushirikiano kati ya Ufaransa na Afrika, hatutaingilia kati wakati kunapotokea mapinduzi barani Afrika" hata hivyo ameongeza Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa alitangaza katikati ya mwezi Septemba kwamba balozi wa Ufaransa nchini Niger alichukuliwa kama "mateka" na jeshi lililoko madarakani na alikuwa akila "mgao wa kijeshi". Viongozi hao wa mapinduzi, ambao walimpindua rais Mohamed Bazoum na kuchukua mamlaka mnamo Julai 26, waliagiza kufukuzwa kwa balozi wa Ufaransa mwishoni mwa mwezi Agosti, baada ya Paris kukataa kufuata makataa ya kumtaka aondoke. Hapo awali Ufaransa ilipinga kuondoka kwa balozi wake nchini Niger kwa wiki kadhaa, ikisema kuwa serikali iliyoko mamlakani haikuwa na mamlaka ya msingi ya kutoa ombi kama hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.