Pata taarifa kuu

Niger: Waziri Blinken amefanya mazungumzo na rais Bazoum aliyeondolewa madarakani

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, amezungumza kwa njia ya simu na rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum kusisitiza uungawaji mkono wa Washington kwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Utawala wa rais Bazoum uliangushwa kupitia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 26 ya mwezi Julai ambapo yeye na familia yake wamekuwa wakizuiliwa
Utawala wa rais Bazoum uliangushwa kupitia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 26 ya mwezi Julai ambapo yeye na familia yake wamekuwa wakizuiliwa © Michel Euler / AP
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa rais Bazoum uliangushwa kupitia mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 26 ya mwezi Julai ambapo yeye na familia yake wamekuwa wakizuiliwa.

Marekani imetoa wito wa kuachiwa huru kwa wahusika wote wanaozuiliwa kinyume cha sheria tangu kufanyika kwa mapinduzi hayo.

Jeshi, chini ya uongozi wa Jenerali Abdourahmane Tchiani, limetangaza serikali ya mpito na kutangaza kipindi cha mpito cha miaka mitatu, hatua ambayo imepingwa vikali na tume ya Ecowas.

Ecowas imekuwa ikijaribu kufanya mazungumzo na utawala wa kijeshi wa Niger kuhusu kurejeshwa kwa utawala wa kiraia na kwa wakati mmoja ilitishia kutumia nguvu za kijeshi kumrejesha madarakani rais Bazoum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.