Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Marekani yataja unyakuzi wa kijeshi nchini Niger kuwa ni mapinduzi na kukata misaada yake

Marekani imeelezea rasmi hatu ya unyakuzi wa madaraka nchini Niger mwezi Julai kama mapinduzi ya kijeshi na hivyo kutangaza kusitisha msaada wa kiuchumi wa dola milioni 442. "Tunachukua hatua hii kwa sababu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita tumetumia njia zote zilizopo ili kuhifadhi utawala wa kikatiba nchini Niger," afisa mkuu wa Marekani amewaambia waandishi wa habari.

Mnamo Julai 26, jeshi lilimwondoa madarakani na kumweka kizuizini rais mteule Mohamed Bazoum, hapa akiwa mapoja na Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.
Mnamo Julai 26, jeshi lilimwondoa madarakani na kumweka kizuizini rais mteule Mohamed Bazoum, hapa akiwa mapoja na Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. © AP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Julai 26, jeshi lilimwondoa madarakani na kumweka kizuizini rais aliyechaguliwa, Mohamed Bazoum.

Afisa huyo mkuu wa Marekani amesema kuwa chini ya sheria za Marekani, viongozi hao wapya walipaswa kurejesha utawala wa kiraia, wa kidemokrasia ndani ya siku 90 hadi 120. "Baada ya muda, ilionekana wazi ... kwamba hawakutaka kuheshimu sheria hizi za kikatiba," ameongeza.

Chini ya sheria ya Marekani, kutajwa unyakuzi wa madaraka kama mapinduzi ya kijeshi kunaashiria kukatishwa kwa misaada kwa nchi husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.