Pata taarifa kuu

Niger: Kuondoka kwa jeshi la Ufaransa kutafanyika 'kulingana na masharti yetu'

Utawala wa kijeshi ulioko madarakani nchini Niger umehakikisha Alhamisi kwamba zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa, ambao limeanza leo alhamisi kulingana na makao makuu ya jeshi la Ufaransa, litatekelezwa kulingana na "masharti" yake na kwa kuzingatia "maslahi" yake.

Wanajeshi 1,000 wa Ufaransa walitumwa katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu", eneo wanakojificha wapiganaji wa kundi la Islamic State.
Wanajeshi 1,000 wa Ufaransa walitumwa katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu", eneo wanakojificha wapiganaji wa kundi la Islamic State. © AP
Matangazo ya kibiashara

 

Katika mchakato huo, Baraza la Kitaifa la ulinzi wa taifa (CNSP, wanajeshi walio madarakani) limethibitisha tangazo hili katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

"CNSP na serikali ya Niger itahakikisha kwamba zoezi hili linafanyika kwa kuzingatia maslahi yetu na kulingana na masharti yetu," inabainisha taarifa. "Wanajeshi 400 wa Ufaransa walioko Ouallam (magharibi) watakuwa wa kwanza kuanza kuondoka nchini Niger. kambi ya kikosi cha wanaanga katika mji mkuuwa Niger, Niamey, ambako wanajeshi wengi wa Ufaransa wamewekwa itavunjwa mwishoni mwa mwaka huu," taarifa hii kwa vyombo vya habari inaendelea.

Makao makuu ya jeshi la Ufaransa ilibaini Alhamisi asubuhi, "kuanzisha operesheni ya kuwaondoa wanajeshi wake ndani ya wiki moja, kwa utaratibu mzuri, kwa usalama na kwa uratibu na mamlaka ya Niger". Uamuzi huu unakuja baada ya mvutano wa zaidi ya miezi miwili na utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi ya Julai 26 dhidi ya rais Mohamed Bazoum.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza mnamo Septemba 24 kumalizika kwa ushirikiano wa kijeshi na Niger na kuondoka hatua kwa hatua kwa wanajeshi wa Ufaransa waliopo katika nchi hii ya Sahel, "mwishoni mwa mwaka", ikiwa ni matakwa kutoka kwa mamlaka mpya ya Niamey.

Wanajeshi 1,000 wa Ufaransa na wanajeshi wa anga wametumwa katika kambi ya anga ya Ufaransa huko Niamey na 400 huko Ouallam na Ayorou (kaskazini-magharibi), wakisaidia wanajeshi wa Niger, katikakatika eneo linalojulikana kama "mipaka mitatu" kati ya Niger, Burkina Faso na Mali, eneo wanakojificha wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.