Pata taarifa kuu

Ufaransa yaanza kuondoa wanajeshi wake nchini Niger

Zoezi la kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa Niger lililotangazwa na Emmanuel Macron mnamo Septemba 24 linaanza Alhamisi hii, Oktoba 5. Kwa mujibu wa jeshi la Ufaransa, muda unahesabilika kwani zozi la kuwaondoa wanajeshi 1,500 wa Ufaransa linapaswa kukamilika ifikapo mwisho wa mwaka wa 2023.

Wanajeshi wa Ufaransa katika kambi ya kijeshi mjini Niamey nchini Niger, Juni 2021.
Wanajeshi wa Ufaransa katika kambi ya kijeshi mjini Niamey nchini Niger, Juni 2021. © AP/Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Kundi la kwanza la wanajeshi 400 wa Ufaransa waliotumwa Ouallam, kwenye mpaka wa Malo na Nigeria, ndio ambao wameondoka. Wanajeshi hawa walishiriki katika Operesheni Almahaou na wanajeshi wa Niger, ili kutoa ulinzi wa Liptako, nchini Niger.

Waajrshi hao ambao wamepangwa katika makundi mawili, huko Ouallam na Tabaré Baré, watasafiri magari yao hadi mji mkuu Niamey na kisha kuandaa safari yao kuelekea nchini Ufarasa. Wataweka magari yao ya kivita katika utaratibu na kufafanua barabara ambayo itabidi kulindwa ili kufikia mji mkuu wa Niger. Umbali sio mrefu sana - karibu kilomita mia kadhaa- lakini kutokana na hali ya barabara, safari inaweza kuchukua siku mbili. Mara baada ya kuwasili katika kambi ya  kikosi cha wanaanga mjini Niamey, wanajeshi hawa 400 wataanza safari yao kwa ndege hadi nchini Ufaransa. “Katika suala la udereva, tutafanya kile kilichopangwa. Tutapanga jinsi ya kuondoka kwa utaratibu mzuri, kwa usalama na kwa uratibu na mamlaka za ndani,” wamebaini maafisa wakuu.

Makao makuu ya jeshi la Ufaransa hawazungumzi chochote kuhusiana na taarifa za utawala wa kijeshi wa Niger ambapo katika siku za hivi karibuni ulitangaza kwamba uratibu huu wa kiufundi hauzingatiwi.

Zoezi la kuwaondoa wanajeshi katika kambi ya wanaanga anga ya Niamey (BAP) litachukuwa muda wa miezi mitatu pekee. Wanjeshi elfu moja wako hapo wanasubiri kuondoka, huku wakiwa wamezungukwa na mamia ya vyombo. Ikiwa wanajeshi wengi wataondolewa kwa ndege, kwa upande mwingine, sehemu nzito zaidi ya mizigo itaondolewa kwa magari.

Wanajeshi wa Ufaransa lazima wawe wameondoka Niger kufikia mwisho wa mwaka. Kwa hivyo jeshi la Ufaransa lazima litafute kitovu cha usafirishaji nje ya Niger ili kuweka kati vifaa vilivyohamishwa kabla ya kuvirudisha Ufaransa. Bandari ya Cotonou ingetumiwa kwa usafirishaji huu, lakini kwa sasa utawala wa kijeshi nchini Niger hauonekani kuwa tayari kufungua mpaka wake na Benin kwa misafara ya kijeshi ya Ufaransa.

Kwa hivyo, usafirishaji wa mizingo na magari mazito ya kijeshi ya Ufaransa unaweza kuwa ngumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.