Pata taarifa kuu

Niger: Maombolezo ya siku tatu baada ya kuuawa kwa wanajeshi 29 yanaendelea

Nairobi – Niger imeanza siku tatu ya maombolezo ya kitaifa, baada ya kuuawa kwa wanajeshi 29 walioshambuliwa na wanajihadi, katika shambvulio baya kuwahi kutokea nchini humo baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi Julai.

Wanajeshi hao wa Niger, walishambuliwa katika eneo la Tabatol, inayopakana na nchi ya Mali
Wanajeshi hao wa Niger, walishambuliwa katika eneo la Tabatol, inayopakana na nchi ya Mali AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja kufuatia shambulio hilo lililotokea Magharibi mwa Niger, baada ya msafara wa wanajeshi hao kushambuliwa na mamia ya wanajihadi waliowarushia vilipuzi.

Serikali ya kijeshi inasema  maafisa wengine wawili walijeruhiwa, huku wanajihadi zaidia ya 10 wakiuawa.

Wanajeshi hao wa Niger, walishambuliwa katika eneo la Tabatol, inayopakana na nchi ya Mali, katika eneo ambalo limeendelea kushuhudia utovu wa usalama.

Kumekuwa na ongezeko la mashambulio dhidi ya maafisa wa usalama katika nchi za Sahel, kwa kipindi cha zaidi ya  miaka 10 sasa, yaliyoanzia Kaskazini mwa Mali na baadaye kusambaa nchini Niger na Burkina Faso.

Nchi za Niger na Mali, zimetaka vikosi vya kigeni, vile vya Ufaransa na Umoja wa Mataifa, kuondoka katika nchi zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.