Pata taarifa kuu

Niger yasitisha mauzo yake ya LPG ili kupendelea soko la kitaifa

Mamlaka ya kijeshi iliyo madarakani nchini Niger imeamua kusimamisha mauzo ya gesi ya petroli (LPG) "hadi itakapochukuliwa hatua nyingine", ili kupendelea usambazaji wa kitaifa, kulingana na hati rasmi ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi siku ya Jumatano.

Niger inakabiliwa na vikwazo vikali kutoka ECOWAS, kufuatia mapinduzi yaliyoweka jeshi mamlakani mnamo Julai 26.
Niger inakabiliwa na vikwazo vikali kutoka ECOWAS, kufuatia mapinduzi yaliyoweka jeshi mamlakani mnamo Julai 26. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Niger ilianza uzalishaji wa LPG mwaka 2012, na kufikia zaidi ya tani 60,000 mwaka 2020, kulingana na takwimu rasmi. Inatumika hasa nchini kwa kupikia.

"Usafirishaji wa gesi nje ya nchi ni marufuku isipokuwa kwa idhini maalum, na hadi itakapochukuliwa hatua nyingine," inabainisha barua kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Forodha, Abou Oubandawaki, iliyoelekezwa kwa idara zake.

"Madhumuni ya agizo hili ni kuzuia usafirishaji wa gesi ya LPG kutoka nchini Niger. Uzalishaji wa kitaifa wa gesi ya LPG kimsingi unahakikisha usambazaji wa soko la kitaifa", inathibitisha agizo kutoka kwa Wizara ya Biashara na Viwanda, la tarehe 25 Septemba.

Kulingana na ripoti kutoka kwa Wizara ya Mafuta, usafirishaji wa LPG "ulikuwa muhimu hasa mnamo mwaka 2013 na 2014", kabla ya kuwa "karibu sifuri mnamo mwaka 2019 na 2020" kwa "ongezeko la mahitaji ya ndani".

Serikali ya Niger ilikuwa imetoa ruzuku kwa LPG ili kukatisha kuzuia matumizi mabaya ya kuni, zinazotumika sana kupikia chakula nchini humo, na hivyo kupambana dhidi ya kuenea ukataji miti.

Niger inakabiliwa kwa miezi miwili na vikwazo vikali kutoka kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), kufuatia mapinduzi yaliyoingiza jeshi madarakani mnamo Julai 26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.