Pata taarifa kuu

Nigeria : Watu 40 wanahofiwa kufariki katika ajali ya boti

Nairobi – Watu 40 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wanasafiria, kuzama katika jimbo la Kebbi, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Watu wengine 10 waliuawa, wakati boti iliyokuwa inasafirisha wafanyabiashara pia kuzama, katika jimbo la Adamawa mwezi Septemba
Watu wengine 10 waliuawa, wakati boti iliyokuwa inasafirisha wafanyabiashara pia kuzama, katika jimbo la Adamawa mwezi Septemba AFP/François Xavier Marit
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa serikali wanasema wanaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao, lakini hawana matumaini iwapo abiria hao watapatikana wakiwa hai.

Bala Mohammed, Mkuu wa Wilaya ya Yauri amesema, msako huo ni mgumu kwa sababu ya kiwango kikubwa kwenye  mto Niger, kilichochangiwa pia na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Ajali za boti hutokea sana nchini Nigeria kwa sababu ya kusafirisha abiria kupita kiasi, mafuriko na kutofanyika kwa ukarabati wa boti.

Mwezi uliopita, watu wengine 24 waliouawa na wengine zaidi ya 50 kutoweka wakati wakulima zaidi ya 100 walipokuwa wanasafiri katika mto Niger, wakati boti yao ilipozama.

Watu wengine 10 waliuawa, wakati boti iliyokuwa inasafirisha wafanyabiashara pia kuzama, katika jimbo la Adamawa mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.