Pata taarifa kuu

Niger: Wanajeshi 29 wameuawa katika shambulio la kijihadi

Nairobi – Wizara ya ulinzi ya Niger imesema wanajeshi wake 29 wameuawa katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na makundi la wanajihadi Magharibi mwa taifa hilo.

Shambulio hili limetajwa kuwa kubwa zaidi nchini humo tangu jeshi kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai
Shambulio hili limetajwa kuwa kubwa zaidi nchini humo tangu jeshi kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili limetajwa kuwa kubwa zaidi nchini humo tangu jeshi kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai.

Katika taarifa iliyotolewa kwa njia ya televisheni, mamlaka nchini Niger imesema vikosi vyake vilishambuliwa na zaidi ya wanajihadi 100 waliokuwa wamejihami kwa bunduki na vilipuzi.

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kuwaomboleza maofisa hao waliouawa wakilinda taifa lao.

Mashambulio yanayotekelezwa na makundi ya kijihadi dhidi ya vikosi vya usalama yamekuwa yakiongezeka tangu jeshi kuchukua madaraka.

Licha ya mashambulio hayo, serikali ya kijeshi kwa upande wake imeahidi kupambana na kumaliza makundi hayo ya watu wenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.