Pata taarifa kuu

ECOWAS yaombwa kulegeza vikwazo ili msaada wa kibinadamu uweze kuingia Niger

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa yanayofanya kazi nchini Niger yameiomba siku ya Jumanne Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kulegeza vikwazo vyake dhidi ya Niamey ili kuwezesha kuingia kwa msaada wa dharura wa kibinadamu kupitia nchi jirani ya Benin.

Mwishoni mwa mkutano wa kilele wa Jumapili mjini Abuja, ECOWAS ilidumisha vikwazo vyake vya kiuchumi na kifedha vilivyowekewa dhidi ya Niger baada ya mapinduzi ya Julai 26, na kusema kulegezwa kwa vikwazo hivyo kutaendana na  "kipindi kifupi cha mpitoi" hasa ili kuwezesha raia kurejea madarakani.
Mwishoni mwa mkutano wa kilele wa Jumapili mjini Abuja, ECOWAS ilidumisha vikwazo vyake vya kiuchumi na kifedha vilivyowekewa dhidi ya Niger baada ya mapinduzi ya Julai 26, na kusema kulegezwa kwa vikwazo hivyo kutaendana na "kipindi kifupi cha mpitoi" hasa ili kuwezesha raia kurejea madarakani. © AP - Chinedu Asadu Chinedu Asadu
Matangazo ya kibiashara

Mashirika haya zaidi ya ishirini yanaomba hasa "kufunguliwa tena mara moja" kwa mpaka na Benin, uliyofungwa kutokana na vikwazo vya kikanda, kuwezesha kuingia kwa misaada ya kibinadamu nchini Niger, ambako zaidi ya watu milioni 4.3 wanahitaji msaada wa haraka kulingana na mashirika hayo.

Mwishoni mwa mkutano wa kilele wa Jumapili mjini Abuja, ECOWAS ilidumisha vikwazo vyake vya kiuchumi na kifedha vilivyowekewa dhidi ya Niger baada ya mapinduzi ya Julai 26, na kusema kulegezwa kwa vikwazo hivyo kutaendana na  "kipindi kifupi cha mpitoi" hasa ili kuwezesha raia kurejea madarakani.

"Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa ya Niger yanaonyesha kusikitishwa kwao na kutokuwepo kwa misamaha ya kibinadamu kutoka ECOWAS kwa vikwazo vilivyochukuliwa dhidi ya Niger", mashirika haya yakiwemo Acted, Oxfam,  NRC na Médecins du Monde yamelaani katika taarifa. "Tunataka kufunguliwa mara moja kwa mpaka kati ya Benin na Niger kwa misaada ya kibinadamu", yanasihi mashirika haya yasiyo ya kiserikali ambayo yanasikitika kwamba ECOWAS "haijazingatia wito" wa jumuiya yza misaada ya kibinadamu "kuhakikisha kwamba raia nchini Niger wanapata huduma muhimu.

Kulingana na Mohammed Chikhaoui, mwakilishi wa mashirika hayo yanayofanyakazi nchini Niger, zaidi ya watu milioni 2 walikabiliwa na uhaba wa chakula kati ya mwezi Oktoba na Desemba 2023, hali ambayo iliwalazimu 15% ya watu kuhama kutokana na ukosefu wa chakula au msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.