Pata taarifa kuu

Niger: Jenerali Tiani azuru Lome siku mbili kabla ya mkutano wa kilele wa ECOWAS

Jenerali Abdourahamane Tiani, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Niger, alizuru Togo Ijumaa, Desemba 8. Ziara hii inakuja siku mbili kabla ya mkutano wa kilele wa ECOWAS siku ya Jumapili mjini Abuja, na wakati nchi hii ikiwa chini ya vikwazo vya jumuiya hii baada ya mapinduzi ya Julai 26. Jenerali Abdourahamane aliandamana hasa na Mawaziri wake wa Ulinzi na Mambo ya Kigeni, akijibu mwaliko wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé, ambaye mamlaka mpya ya Niger ilimtaka kuchukua jukumu la mpatanishi.

Jenerali Abdourahmane Tiani akiwasili kukutana na mawaziri huko Niamey, Niger, Julai 28, 2023.
Jenerali Abdourahmane Tiani akiwasili kukutana na mawaziri huko Niamey, Niger, Julai 28, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Haijalishi ni mgogoro gani, suluhu huwa katika mazungumzo," Jenerali Tiani alitangaza kwa wanadiaspora wa Niger huko Lomé, mji mkuu wa Togo, inayotajwa kama nchi ndugu, kama Mali na Burkina Faso. 

Ziara ya kikazi, kwa mwaliko wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé, ambaye alikutana ana kwa ana na mkuu wa CNSP, siku mbili kabla ya mkutano wa kilele wa ECOWAS mjini Abuja, Jumapili Desemba 10. Mkutano huu wa kilele unaelezewa kuwa wa "maamuzi" na mamlaka mpya ya Niger, ambao wanatumai kuona vikwazo vikiondolewa, na "wanategemea uungwaji mkono wa Togo", kama walivyoandika kwenye mitandao ya kijamii.

Mwezi mmoja uliopita, Niger iliiomba Togo kuchukua nafasi ya mpatanishi na nchi za Afrika Magharibi. Hiki ni kitendo cha kusawazisha kwa Togo, ikilinganishwa na wenzao wa ECOWAS. Hii ni kutafuta suluhisho la pamoja linalofaa pande zote. Lakini pia katika mizani, huko Abuja, hatima ya rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum, anayezuiliwa katika makao ya rais na mkewe na mwanawe tangu mapinduzi.

Baada ya ziara hii, ufunguzi wa ubalozi wa Togo mjini Niamey ulitangazwa, na ziara ijayo ya Faure Gnassingbé nchini Niger, ambayo tarehe yake bado haijajulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.