Pata taarifa kuu

Utawala wa kijeshi wa Niger unaiomba Togo kuwa mpatanishi

Utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi nchini Niger umeiomba Togo kuwa mpatanishi katika mazungumzo yake na jumuiya ya kimataifa, hususan na nchi za Afrika Magharibi ambazo ziliichukulia vikwazo majira ya joto mwaka huu.

Rais wa Togo Faure Gnassingbé, Februari 17, 2020.
Rais wa Togo Faure Gnassingbé, Februari 17, 2020. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Niger Jenerali Salifou Moby alikutana mchana na Rais wa Togo Faure Gnassingbé katika mji mkuu wa Togo Lomé.

Baada ya mapinduzi ya Julai 26, Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) iliiwekea Niger vikwazo vikali vya kifedha ili kushinikiza jeshi lililompindua rais mteule Mohamed Bazoum kurejesha madaraka. Jenerali Mody alishutumu vikwazo hivi "vya kijinga", na akaishukuru Togo kwa kuendelea kuzungumza na utawala wa kijeshi baada ya mapinduzi, tofauti na nchi nyingine nyingi.

Ingawa ni mwanachama wa ECOWAS, Togo imechukua hatua kadhaa za nchi mbili kufanya mazungumzo na utawala wa kijeshi wa Niger. "Hatujawahi kufunga nchi yetu kwa marafiki zetu (...) Niger inasalia wazi, hata kama mipango imefanywa ili tusiweze tena kuzungumza nao," Jenerali Mody ametangaza kwa waandishi wa habari baada ya mkutano wake na Rais Gnassingbé. "Tulimwomba Rais wa Jamhuri ya Togo kuwa mpatanishi, ili kuwezesha mazungumzo haya na washirika wetu mbalimbali," ameongeza.

Ufaransa, ukoloni wa zamani wa Niger, ulihusika katika mvutano na utawala wa kijeshi baada ya mapinduzi, kisha ulianza Oktoba, kwa ombi lake, kuwaondoa takriban wanajeshi 1,500 waliotumwa nchini humo.

"Tunaiomba Togo, nchi yetu rafiki, kwa kuzingatia kile inachoendelea kutupa, kuwa mdhamini wetu" ndani ya mfumo wa makubaliano ya uondoaji wa kijeshi wa Ufaransa, ambao "unaendelea" na unafanyika "kawaida" ameongeza Jenerali Mody. .

Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo, Robert Dussey, kwa upande wake amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba nchi yake iko tayari "kusaidia kama mwezeshaji" katika mazungumzo kati ya Niger na jumuiya ya kimataifa, akimshukuru Jenerali Mody "kuteua, pamoja na Marekani, Togo kama nchi iliyodhamini uondoaji wa majeshi ya Ufaransa."

Utawala wa kijeshi mjini Niamey umekataa madai kutoka kwa ECOWAS ya kurejesha utawala wa kikatiba, na unasisitiza juu ya haja ya muda wa mpito wa miaka mitatu zaidi kufanya hivyo, wakati nchi hiyo inakabiliwa na makundi mawili ya waasi ya wanajihadi kusini mashariki na magharibi.

Togo mara kwa mara hujaribu kujiweka kama mpatanishi katika eneo hilo. Mnamo 2022, ilishiriki hasa katika juhudi za kuwaachilia huru wanajeshi 49 wa Côte d'Ivoire waliokuwa walizuiliwa huko Bamako, Mali, baada ya kushutumiwa kuwa mamluki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.