Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya waanza hatua za kuiwekea vikwazo serikali ya kijeshi ya Niger

Umoja wa Ulaya umeanza hatua za kuwawekea vikwazo wanachama wa utawala wa kijeshi nchini Niger, miezi mitatu baada ya kuchukua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi.

Kikosi cha polisi kikishika doria ya mjini Niamey nchini Niger.
Kikosi cha polisi kikishika doria ya mjini Niamey nchini Niger. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Baraza la EU limetangaza kwamba limepitisha mfumo ambao utaliruhusu kuweka vikwazo dhidi ya watu binafsi na vyombo vinavyohusika na vitendo vinavyotishia amani, utulivu na usalama nchini Niger.

Aidha Baraza hilo limeongeza kuwa vikwazo hivyo vitawekewa watu binafsi ambao wanahujumu utaratibu wa kikatiba wa Niger, demokrasia au utawala wa sheria, pamoja na watu binafsi wanaohusika na ukiukaji wa haki za binadamu.

Vikwazo hivyo vitajumuisha marufuku ya usafiri, kufungia mali na kupiga marufuku utoaji wa fedha kwa watu waliowekewa vikwazo.

EU, hata hivyo, ilisema kwamba itakubali msamaha wa kibinadamu kwa hatua za kufungia mali.

Hatua hiyo ya Ulaya inafuatia Niger kuwekewa vikwazo na Ecowas na kusitishwa kwa misaada na serikali ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.