Pata taarifa kuu

Niger: ECOWAS yafungua njia ya kulegeza vikwazo chini ya masharti

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), iliyokutana katika mkutano wa kilele mjini Abuja, imefungua njia ya kulegezwa kwa vikazo dhidi ya Niger, kwa kuiwekea "kipindi kifupi cha mpito" kabla ya raia kurejea madarakani.

Kikao cha 64 cha kisicho kuwa cha kawaida cha wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mjini Abuja mnamo Desemba 10, 2023.
Kikao cha 64 cha kisicho kuwa cha kawaida cha wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mjini Abuja mnamo Desemba 10, 2023. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Kamati inayoundwa na marais wa Benin, Togo na Sierra Leone itajadiliana na utawala wa kijeshi wa Niger kuhusu ahadi za kutekelezwa kabla ya uwezekano wa kulegeza vikwazo, ametangaza Mwenyekiti wa tume ya ECOWAS, Omar Touray.

Wanajeshi hawa, waliompindua rais mteule Mohamed Bazoum katika mapinduzi ya Julai 26, wametawala nchi hiyo ndani ya Baraza la Kitaifa la Ulinzi wa taifa (CNSP).

Kwa kujibu, mwanzoni mwa mwezi Agosti, wanachama wa ECOWAS waliweka vikwazo vizito vya kiuchumi na kifedha kwa Niamey.

"Kulingana na matokeo ya ushirikiano wa kamati ya wakuu wa nchi na CNSP, mamlaka itapunguza hatua kwa hatua vikwazo vilivyowekwa kwa Niger," Bw. Touray ametangaza baada ya mkutano huo. Lakini "kama CNSP haitazingatia matokeo ya ushirikiano na kamati, ECOWAS itadumisha vikwazo vyote," ameongeza.

Shirika la kikanda linitaka Niamey kujitolea kwa "kipindi kifupi cha mpito" kuelekea "marejesho ya haraka ya utaratibu wa kikatiba", au kurejea kwa utawala wa kiraia.

Jukumu la mpatanishi

Uamuzi huu wa ECOWAS unafuatia ziara nchini Togo siku ya Ijumaa ya kiongozi wa kijeshi wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, akiwa na baadhi ya mawaziri wake. Siku chache kabla, Niamey ilimwomba Rais wa Togo Faure Gnassingbé kuchukua nafasi ya mpatanishi.

"Tiani yuko tayari kujadili muda wa kipindi cha mpito na hali ya Bazoum," ambaye ametengwa huko Niamey katika makazi yake tangu Julai 26, kimesema chanzo cha Togo kuhusu majadiliano haya.

Katika ufunguzi wa mkutano huo, Bw. Touray alitangaza kwamba "mamlaka za kijeshi (huko Niamey) kwa bahati mbaya zimeonyesha wasiwasi wake kwa kung'ang'ania misimamo yao isiyokubalika, na kuchukua mateka sio tu rais Bazoum, familia yake na wajumbe wa serikali yake, lakini pia raia wa Niger.

Siku ya Jumapili msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Molly Phee, alisema kwamba amealikwa kushiriki katika mijadala ya kilele yenye lengo la kuwezesha kurudi kwa utawala wa kidemokrasia nchini Niger na kusaidia kuifanya Sahel kuendelea zaidi.

Kihistoria mshirika mkuu wa nchi za Magharibi katika mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi, Niger imetaka kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa ambao tayari zoezi hilo limeanza, wakati Marekani bado ina wanajeshi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.